• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAFUGAJI WAHAMASISHWA KUTUMIA MBEGU BORA ZA MALISHO ILI KULETA TIJA KWENYE MIFUGO

Imetumwa : August 5th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepiga hatua katika kuongeza upatikanaji wa mbegu bora za malisho ya kupandwa (majani) yanayoleta tija kwa Wafugaji kutokana na kuifanya Mifugo kuwa na uzito mkubwa unaoongeza thamani yake sokoni na kuthibitisha kauli mbiu ya 'Ufugaji ni utajiri'.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo aliposhiriki Maonesho ya Gwaride (Paredi) la Wanyama lililofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma sanjari na Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2025 Kanda ya Kati, leo Agosti 05, 2025.

"Sasa hivi Wafugaji wameanza kuelewa umuhimu wa kutumia majani ya kupandwa kwa ajili ya Mifugo au malisho, hatua hii ni kubwa na tunaipongeza sana na sasa tumeona Wizara imepanga kuendeleza upatikanaji wa mbegu bora. Yote haya yanafanywa ili wafugaji waweze kupata uwezeshaji”.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin P. Mhede ametoa wito kwa Wafugaji na Wavuvi kwa niaba ya Wizara yake, kuchangamkia fursa za matumizi ya teknolojia zinazooneshwa kwenye Maonesho ya mwaka huu ambazo zimeendelea kusanifiwa na Wataalam ili mwakani sekta hiyo iweze kuja na matokeo makubwa zaidi.

Hata hivyo, Mdhamini Mkuu wa Gwaride hilo mwaka huu, Benki ya TCB, ikiwakilishwa na Bw. Frank Kipalamoto kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, amesema Taasisi hiyo imedhamini kuletwa kwa vijana 150 kutoka mikoa 12 ya Tanzania ambao ni wafugaji wa Kuku kwa lengo la kujifunza ufugaji wa kisasa utakaowaongeza tija pindi watakaporejea makwao.

Akizungumzia Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo kwa Mifugo, Dr. Benezet Lutege amesema Serikali imeridhia jumla ya shilingi Bilioni 216 kwa ajili ya kuendesha kampeni hiyo na utambuzi wa Mifugo nchi nzima ambapo takribani Ng’ombe Milioni 19, Mbuzi na Kondoo Milioni 17 pamoja na Kuku Milioni 40 zitapatiwa chanjo hiyo huku Mifugo zaidi ya 1,000 ikiwa imeshachanjwa viwanjani hapo.

Gwaride la Mifugo 2025, ni la 14 tangu kuasisiwa kwenye kilele cha Maonesho ya Nanenane 2010, likilenga kuhamasisha matumizi ya Teknolojia katika shughuli za ufugaji ili kupata mazao bora ya Mifugo yanayokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa sambamba na kuunganisha Wafugaji na Wataalam wa mafunzo ya Ugani kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Kaulimbiu: “Chagua Viongozi Bora Kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.


#nanenanekitaifa2025kandayakati

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.