• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI

Imetumwa : January 29th, 2025

Na. Sizah Kangalawe 

Habari- Dodoma Rs.

Miongoni mwa sifa ya mzalendo ni Kuwafundisha na kuwahamasisha watu wake wa karibu kama familia, ndugu, majirani na marafiki kuipenda nchi yao na kujitoa kwa ajili yake pamoja na kuwafundisha watoto tamaduni za nchi husika.

Somo la uzalendo linapaswa kufundishwa Kwa Rika zote ikiwemo wanafunzi mashuleni, ndio maana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaagiza Walimu wa shule za Mkoani hapa  Kuwafundisha wanafunzi uzalendo pindi tu wanapojiunga na shule Kwa ngazi ya awali na kuendelea.

Maagizo hayo ameyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Bahi katika shule ya Msingi Kusila na shule ya Sekondari Mwitikira alipotembelea kujionea utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu katika shule hizo.

Mhe. Senyamule Amesema " Suala la uzalendo lazima lihimizwe shuleni,  ndio maana tuliagiza nyimbo za Taifa ziimbwe Kila siku, Sina hakika kama mnatekeleza kama tulivyokubaliana. Hawa watoto pamoja na kufaulu kwao lakini tunataka viongozi waaminifu na wanaoipenda nchi yao ya Tanzania.

"Kwa vyovyote vile, hayo yote yanafundishwa shuleni kwa hiyo, Walimu jitahidini kuwakazia sana juu ya uzalendo, anzieni Kuwafundisha tangu wakiwa madarasa ya chini kabisa na sio la 6 & 7 Ili wayashike katika umri ambao wataalam wanapendekeza kuwa mtoto anakuwa na uelewa wa kushika vitu Kwa haraka kati ya miaka 4-7 na sio rahisi kwao kusahau Kwa haraka", Amesema Senyamule

Katika hatua nyingine RC Senyamule ameuomba uongozi wa Kijiji Cha Kusila, kuandaa Mpango mzuri utakaowawezesha kujenga angalau maboma mawili na wakifika katika hatua ya umaliziaji Serikali ya Wilaya itakamilisha majengo hayo Kwa hatua za mwisho Ili kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa unaoikabili shule hiyo.

Hata hivyo umefanyika mkutano wa hadhara katika kata ya Mwitikira ambapo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Victor Swela ametumia Fursa hiyo kuwaasa wananchi kuachana na vitendo vya rushwa na kutoa taarifa pindi wanapobaini viashiria vya adui huyo wa haki Ili waweze Lusitania kazi Kwa wakati.

Kutokana na kijiji Cha Mwitikira kuwa pembezoni mwa Wilaya hiyo mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Peter Madialo ameuomba uongozi wa Mkoa kuwajengea kituo Cha polisi kijijini hapo Ili kuimarisha Hali ya Usalama ambapo Mkuu wa Mkoa ameahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji Ili kukamilisha kituo hicho na kuahidi kuwa pindi watakapoanza ujenzi huo ndipo atawakabidhi saruji hiyo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.