• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAFUNZI 571 WATAJWA KUNUFAIKA NA PROGRAM WEZESHI YA MEMKWA DODOMA

Imetumwa : August 18th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Takribani wanafunzi 571 wamenufaika na program wezeshi ya MEMKWA ndani ya Mkoa wa Dodoma iliyoanzishwa na Serikali kwa dhumuni la kumuwezesha Mtanzania ambaye hakubahatika kupata Elimu kupitia Mfumo rasmi kuipata kwa njia mbadala.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akihutubia hadhara wakati wakati wa Maadhimisho ya Juma la Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi yaliyofanyika Agosti 18, 2025 katika Uwanja wa michezo wa Puma Wilayani Kondoa.

“Sote hapa ni mashahidi wa jinsi program hizo zilivyowezesha Watanzania kupata elimu pamoja na ujuzi mbalimbali, MEMKWA, wanafunzi 571 hawa bila kuwepo MEMKWA huenda wasingejua kusoma na kuandika. Elimu ya MASAFA  tumeisikia hapa wanafunzi 355, IPOSA tumesikia wanafunzi 240, program ya MKEJA wanafunzi 1,320”.

Mhe. Senyamule meongeza kuwa, Mkoa umekua na mazingira yaliyoboreshwa ya kujifunzia kusoma, kuandika na kuhesabu kwa usawa na ujumuishi wa makundi yote ikiwemo kundi la wenye mahitaji maalum na Serikali inaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya Elimu kwa kutoa fedha kupitia miradi mbalimbali.

Kadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa amesema wastani wa wanafunzi 1,000 wamenufaika na program hizo za elimu na zimeleta tija na matokeo chanya kwa wanufaika ambapo zimetimiza azma ya Mhe. Rais kumhakikishia mtoto wa kike anapata fursa ya kufikia ndoto zake.

Licha ya hayo, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo, amesema Mkoa umejikita kusimamia na kuratibu elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi kwenye Maeneo ya Uwiano Kati ya Elimu na Jamii (MKEJA) ambapo wana-kisomo wanapata elimu kwa kujifunza maarifa na ujuzi kwenye madarasa maalum yaliyopo kwenye shule za msingi na sekondari.

Maadhimisho ya Elimu ya Watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi yalianzishwa na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni yakiwa na lengo la kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa Elimu ya Watu wazima ambapo Mkoa wa Dodoma huadhimisha kila mwaka kwenye Wilaya iliyochaguliwa.

Kaulimbiu: “Kukuza Kisomo Katika Zama za Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu ya Taifa Letu”


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.