• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

Imetumwa : May 17th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wanafunzi wameaswa kuwa safari ya kutafuta elimu ni ndefu na yenye kuhitaji vipawa na malengo mahsusi ili kuweza kupata mafanikio na maendeleo katika Taifa. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Maria de Mattias.

Katika Mhafali hayo ya 10 yaliyofanyika leo Mei 17, 2025, kwenye ukumbi wa shule hiyo iliyopo Kisasa Jijini Dodoma, Mhe. Senyamule ametoa hotuba yake iliyogusa vipengele kadhaa vyenye kuwausia wanafunzi hao juu ya maisha nje ya shule ambapo aliwekea mkazo suala la elimu.

“Safari iliyopo mbele bado ni ndefu na kubwa, inahitaji vipawa, watu wenye malengo, wachapakazi, wenye bidii kubwa, waaminifu na kwa sababu ni watoto wa kike na kiume, inahitaji watu wanaojitambua na wanaojitunza. Kujitunza ni wajibu wa kila mmoja, lakini inahitaji watu majasiri na wenye ubunifu wa kufanya mambo.”

Hata hivyo, mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Mwl. Justin Machela, amezungumza na wazazi wa wahitimu hao na kuwasisitiza juu ya malezi mema kwa watoto wao ambao bado wanahitaji uangalizi wa karibu wa wazazi kwani sasa wanatoka mikononi mwa Walimu na wanakwenda kuwa chini ya uangalizi wao.

Vilevile, Mkuu wa Shule hiyo Sister Theresia Mkuyi, amewataka Wahitimu kuendelea kuwa na nidhamu, maadili mema na kutumia maarifa waliyopata shuleni hapo kwa manufaa yao binafsi na jamii kwa ujumla, huku wakiwa waangalifu kwenye matumizi ya teknolojia na kuwa Mabalozi wazuri wa shule hiyo.

Shule ya Sekondari Maria de Mattias, ilianzishwa mwaka 2010 chini ya uongozi wa Shirika la Masista wanao abudu Damu ya Kristo ikiwa na wanafunzi 90 wa kidato cha kwanza kwa lengo la kuwalea Wasichana kielimu, kimwili, kiroho na kimaadili. Kwa sasa, shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 535 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.