• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"WASIMAMIZI UJENZI WA MADARASA KONDOA TC MJITATHIMINI"RC SENYAMULE

Imetumwa : November 22nd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule, amefanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa madarasa katika shule mbili za sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Kondoa Mji ambazo ni shule ya sekondari Kwapakacha pamoja na shule ya sekondari Bicha.

Ziara hii ni mwendelezo wa ziara ambazo Mhe. Senyamule amekuwa akifanya katika kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni pamnoja na ujezi wa vyumba vya madarasa na ofisi  kwa shule za shule za sekondari, ambapo Serikali imetoa fedhaili kuwezesha ujenzi huo na Mkoa wa Dododma umepokea fedha zitokazowezesha ujenzi wa madarasa 339.

Katika shule ya sekondari Kwapakacha ambayo imepokea kiasi cha Shilingi Milioni 40 kwa  ajili ya ujenzi wa madarasa 2, ujenzi wa madarasa hayo bado umeonekana kuwa upo nyuma kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na Mkoa kwa makubaliano na wakurugenzi wa Halmashauri zote 8 za Mkoa wa Dodoma kuwa madarasa hayo yatakabidhiwa ifikapo Desemba 5 mwaka huu, ili kuweza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani.

Vivyo hivyo katika shule ya Sekondari ya Bicha, shule hiyo  imepokea Shilingi Milioni 40 kwa  ajili ya ujenzi wa madarasa 2. Bado hali ya Ujenzi hairidhishi licha ya uongozi kuahidi kukamilisha ujenzi na kukabidhi madarasa ifikapo tarehe 25 Novemba,2022.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoawa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka wasimamizi wa ujenzi kwa shule zote mbili kujitathmini upya. "Sijafurahishwa na hali ya miradi inavyoendelea na sidhani kama mnaweza kukabidhi kwa tarehe hiyo mnayoisema hapa. Hebu viongozi mnaosimamia ujenzi huu, mjitathmini kwa kuwa nyuma ya muda, mjipange muwe na mikakati ya kumaliza ujenzi kwa wakati maana hii ni kazi ya Kitaifa ya kujenga madarasa haya" amesema RC Senyamule

Akisoma taarifa ya miradi ya madarasa inavyoendelea katika Halmashauri hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa Mji,Bi. Irene V. Misha amesema kuwa wamepokea Shilingi Milioni 180,000,000/= kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa katika shule Tano za sekondari ikiwa ni pamoja na Kwapakacha vyumba 2, Gulabi chumba 1, Bicha vyumba 2, Ula vyumba 2 na Dilai vyumba 2.

"Halmashauri iliunda timu ya ufuatiliaji wa mradi ambapo kila Mkuu wa Idara alipewa Kata ya kusimamia ambayo ndani yake kuna shule yenye ujenzi wa vyumba vya madarasa.Ufuatiliaji wa kila wiki unafanywa na taarifa ya utekelezaji inawasilishwa kila Jumatatu ya Juma. Hadi kufikia tarehe 17 Novemba, majengo yanayojengwa yamefikia hatua ya upauaji na upigaji wa plasta" Bi Mosha

Awali kabla hajaanza ukaguzi wa madarasa hayo, Mhe Senyamule amezindua rasmi nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa ambayo utekelezaji wa mradi wake ulianza tarehe 11 May 2021 lengo likiwa ni kujenga makazi ya kudumu ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa mradi ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 640,317,900.00 ikijumuisha na VAT. Pamoja na huo Mkuu wa Mkoa Mhe. Senyamule amekagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala Wilaya ,ambapo ujenzi unaoendelea na upo kwenye hatua za umaliziaji.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.