• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATUMISHI WA UMMA MKOA WA DODOMA WAPANDA MITI 988 KUKIJANISHA DODOMA

Imetumwa : December 11th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Katika utekelezaji wa kampeni ya ‘Kijanisha Dodoma’, leo Disemba 10, 2024, Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Watumishi wa  taasisi mbalimbali za Serikali Mkoani hapa,wakiongozwa na Katibu Tawala Mkoa Bw.Kaspar Mmuya, wamepanda miti takribani 988 katika maeneo tofauti Jijini Dodoma.

 “Tumeweza kupanda Miti kando kando ya barabara na maeneo ya wazi, lengo likiwa ni kufanya mji wetu wa Dodoma uonekane msafi, uwe na rangi ya kijani,lakini pia barabara hizo zituzwe ili kuzuia mmomonyoko na kupata kivuli” Bw. Mmuya

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ambaye ameshiriki upandaji miti amesema lengo ni kutunza barabara.

“Tumeona tujielekeze kwenye kuhifadhi barabara zetu na kuzifanya ziwe nadhifu na mandhari nzuri, kwani barabara hizi bado hazijakabidhiwa na zipo kwenye hatua za umaliziaji hivyo tutawasiliana na Wakandarasi ili wafanye kurudisha kwa jamii kwa kuunda vikundi vya uangalizi wa miti hii” Mhe. Shekimweri

Akiongea kwa niaba ya Wakuu wa Taasisi zilizopo katika Mkoa wa Dodoma zilizoshiriki katika zoezi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA Mkoa wa Dodoma Mhandisi Edward Dimelo amesema;

“Miti hii ni muhimu kupandwa kwenye barabara  kwani inasaidia sana kutunza barabara zetu. Wananchi wanaweza kuwa mashahidi kipindi hiki cha mvua, sehemu nyingi zimekua na mmomonyoko wa udongo kwa sababu hakuna miti ila kwa kupanda miti hii, tunakwenda kuzuia mmomonyoko wa udongo na barabara zetu zitakua katika hali nzuri”

Maeneo yaliyopandwa miti katika utekelezaji wa kampeni hiyo ni pembezoni mwa barabara ya Mlimwa C kuzunguka ukuta wa makazi ya Waziri Mkuu yenye urefu wa Km 2.6 ambao imepandwa miti 588 pamoja na barabara ya Bima yenye urefu wa Km 2 iliyopandwa miti 400.


 #dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu        

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.