• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI MKUU AKAGUA UTEKELEZAJI WA KAMPENI YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

Imetumwa : November 7th, 2024

Na. Hellen M. Minja,        

       Habari – DODOMA RS

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, leo Novemba 07, 2024, amefanya ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji wa kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akiwa shuleni hapo, Mhe. Majaliwa amepata nafasi ya kukagua matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambapo shule hiyo inatumia kuni mbadala  kupikia (kuni poa).

“Hapa Msalato nimeona kitu kipya kabisa kinaitwa ‘kuni poa’ zinatokana na takataka, takataka hizo zinachakatwa, zinatengenezwa kwa ustadi mzuri inakua kuni, kuni hii haitokani na kukata miti na kuileta hapa jikoni, inatokana na maganda ya miwa, pumba za mahindi, mtama mabua ya mahindi ndio yanayotumika hapa kuanzia mwaka jana”

“Matumizi ya nishati safi ni ubunifu wa Rais wetu, ambaye amebobea kwenye uhifadhi wa mazingira, aliona kukemea watu wasikate miti, wasichome mkaa pekee haitoshi,badala yake tuhamasishe wananchi watumie gesi, umeme na mkaa mbadala” Amesema Mhe. Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeunda kamati ya Kitaifa inayojumuisha taasisi na viongozi wa wizara mbalimbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Zanzibar, kwa ajili ya kuhamasisha Watanzania kutumia nishati safi, ikilenga taasisi zenye idadi  ya watu kuanzia 100 ziachane na matumizi ya nishati chafu kufikia Desemba 2024.

Hata hivyo, Mhe. Majaliwa amesema kuwa, Taifa limeweka Mkakati wa miaka 10 kuanzia mwaka 2023 hadi 2033, angalau 80% ya Watanzania wawe wanatumia gesi, umeme, mkaa mbadala na kuachana na ukataji miti kwa ajili ya mkaa na kuni, huku fursa zikitangazwa kwa wajasiriamali kuuza majiko ya gesi, umeme, mkaa mbadala na kuni poa.


#kurayakosautiyako  

#ujanjanikupigakura                #dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.