• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WEKENI KIPAUMBELE KUNDELEZA VIJANA-MAJALIWA

Imetumwa : August 8th, 2023


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka viongozi na wataalamu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka kipaumbele katika kuendeleza vijana ili washiriki kikamilifu kwenye shughuli za kuinua uchumi na kuwapatia ujuzi na mbinu za ujasiriamali.

Mhe. Majaliwa amesisitiza kila Mkoa kuandaa mpango mahsusi wa kuhamasisha vijana kufanya shughuli zenye staha na kuwavutia vijana wengi kushiriki shughuli za kiuchumi kwa kuwa Mkoa wa Dodoma umeanza na mingine ijiandae.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Jumanne, Agosti 8, 2023) wakati akifunga Kongamano la Vijana katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Ameagiza vijana kupatiwa mbinu na ujuzi wa ujasiriamali ili waweze kuchangamkia fursa zilizopo mbele yao.

Waziri Mkuu amezitaka Taasisi na Mifuko ya Uwezeshaji kwa vijana kutangaza fursa zilizopo na watumie mbinu mbalimbali zikiwemo redio hasa za kijamii kuwafikia walengwa.

“Kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki katika kuwapa taarifa kuwaongoza na kuwaunganisha na fursa mbalimbali za kukuza mitaji yao.”

“Halmashauri zihakikishe kuwa vijana walio tayari kufanya uwekezaji katika shughuli za uchumi wanapata taarifa za fursa za mitaji. Nyote mlimsikia Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akisisitiza kuhusu kutoa taarifa kwa walengwa.”

Amesema Mikoa iandae utaratibu wa kutoa elimu mtambuka kwa vijana ili kupata stadi za maisha na kufanya maamuzi sahihi, masuala hayo ni pamoja na utunzaji wa mazingira na mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI, maadili, uzalendo, mapambano dhidi ya dawa za kulevya na rushwa.       Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema vijana wote walioshiriki katika kongamano hilo anaamini wameshaiva na wako tayari kwa kazi, hivyo watumie maarifa waliyoyapata kuchangamkia fursa zilizopo ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma. Vilevile, kuwa wadadisi kubaini na kuchangamkia fursa hizo.

”Mmeshapata maarifa mengi kupita kongamano hili wakati umefika sasa mnakwenda kutumia maarifa hayo kwa vitendo. Mikoa nayo iandae utaratibu wa kutoa elimu kuhusu masuala muhimu na mahsusi ya mtambuka kwa vijana ili wapate stadi za maisha na kufanya maamuzi sahihi.”

“Nitoe wito kwenu vijana kuitumia fursa hii muhimu na adhimu mliyoipata katika kongamano hili kuanzisha na kuendeleza miradi yenu na baadaye kuondoa tatizo la ajira na umaskini kwa nchi yetu. Muhimu ni kuthubutu, kuchukua hatua, kuanza kidogo na kukua. Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira njema kuhusu ustawi wa vijana.” Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewahimiza Vijana hao waliofanikiwa kupata mafunzo kuhusu elimu ya kuchangamkia fursa kutoka kwa wabobezi mbalimbali kuhakikisha wanafanyia kazi kwa vitendo bila kuwa na hofu.

Awali ,Mhe.Senyamule alisema kongamano hilo la siku mbili limeshirikisha vijana zaidi ya 3,000 kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma limelenga kuwawezesha vijana hao kutambua fursa za kiuch

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.