KWA UFUPI YALIYOJIRI WAKATI WA ZIARA YA MKUU WA MKOA WA DODOMA DKT. BINILITH SATANO MAHENGE ALIPOTEMBELEA TANESCO MKOANI DODOMA JANUARI 7, 2018
#Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge ameendelea na Ziara yake ya siku nne ya kutembelea Taasisi za Umma zilizopo Mkoani Dodoma ambapo leo ametembelea Tanesco kwa kupata fursa ya kuzungumza na watumishi, kutembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Zuzu na kukagua kituo cha kupokelea na kusambazia umeme kilichopo eneo la Zuzu
#Dkt. Mahenge: Lengo la ziara ni kuona na kutathimini utayari na mipango ya Tanesco ya kuipokea Serikali inapohamia hapa Mkoani Dodoma Makao Makuu kwa upande wa huduma zao za umeme na pia huduma hiyo kwa masuala ya uwekezaji hususani wa viwanda.
#Dkt. Mahenge: Tanesco Dodoma jipangeni kutoa huduma yenye kukidhi mahitaji makubwa zaidi ya hata ilivyo kwa Jiji la Dare es salaam kwa kuwa Dodoma ni Makao Makuu Serikali imehamia, lakini shughuli za kibiashara na huduma mbalimbali zitaongezeka pamoja na uwekezaji mkubwa kama viwanda utaongezeka.
#Dkt. Mahenge: Tanesco Dodoma jengeni hoja ya kuwezeshwa kwa kuongezewa uwezo wa Rasilimali fedha na mahitaji mengine muhimu ili kuboresha Miundombinu ya Upatikanaji umeme wa uhakika na usambazaji kwenye maeneo yote yenye uhitaji hapa Makao Makuu ya Nchi.
#Dkt. Mahenge: Tanesco Dodoma Punguzeni adha ya kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa watumia umeme na wakati mwingine linaleta hasara.
#Dkt. Mahenge: Kama vile Tanesco mnavyojiwekea malengo ya kuunganisha wateja wapya, jiwekeeni malengo ya kuzuia changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, mkifanikiwa hilo mtavutia zaidi wawekezaji maana wao wanatafuta sehemu yenye upatikanaji wa uhakika wa umeme na usiokatikakatika.
#Dkt. Mahenge: Tanesco tubadilike tuwe taasisi yenye kutoa huduma kibiashara kwa kuwa karibu zaidi na wateja, kueleza zaidi mipango ya usambazaji huduma, kushauri maeneo mazuri ya kuwekeza, kutenga fedha za kutosha za miradi ya uwekezaji na kuboresha zaidi huduma ukizingatia hii ni Serikali ya Awamu ya Tano ya Kazi tu.
#Dkt. Mahenge: ameahidi kuisaidia Tanesco katika kukusanya madeni yake kwa kukutana na kuzielekeza taasisi zote zinazodaiwa na Tanesco kulipa madeni yao mara moja.
#Meneja wa Tanesco Kanda ya Kati Mhandisi Athanasius Nangali: Kwa sasa mahitaji ya Umeme kwa Mkoa wa Dodoma Makao Makuu ni 28MW wakati uzalishaji kwa sasa ni Jumla ya 48MW hivyo kuna ziada ya 20MW.
#Mhandisi Athanasius: Mbali na ziada hiyo ya 20MW, Mkoa una kituo kimoja cha Zuzu cha uzalishaji umeme kwa kutumia mafuta chenye uwezo wa kuzalisha 7.4MW ambacho huwa msaada mkubwa wakati wa dharura mara itokeapo hitilafu kwenye Grid ya Taifa, kituo hiki hutumika kusambaza umeme maeneo muhimu hapa Mkoani.
#Mhandisi Athanasius: Tanesco Dodoma inakusanya takribani Tsh 4Bil. kwa mwezi lakini bado hadi kufikia Disemba 2017, Tanesco Dodoma inadai takribani Tsh 2Bil. kutoka kwa wateja binafsi na Taasisi za Serikali, ambapo zoezi la marejesho/malipo linaendelea.
#Mhandisi Athanasius: Miradi ya Umeme Vijijini (REA) awamu ya kwanza ilikamilika mwaka 2012 kwaa vijiji 9 kupata umeme, Awamu ya pili ilikamilika mwaka 2016 kwa vijiji 197 kupata umeme, na Awamu ya tatu ilianza Julai 2017 na inatarajiwa kukamilika Juni 2019 na vijiji 150 vinatarajiwa kupatiwa umeme.
#Mhandisi Athanasius: Ili kutosheleza zaidi mahitaji ya uhamiaji Makao Makuu na Uwezeshaji Viwanda Mkoani Dodoma, Tanesco imepanga miradi ya upanuzi wa miundombinu ya umeme.
#Mhandisi Athanasius: Miradi hiyo inahusisha upanuzi wa kituo cha kupooza umeme cha zuzu, Ujenzi wa njia ya msongo wa KV 132 yenye KM 135, Upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha mjini Kati, Uwekaji Transfoma kubwa kwenye kituo cha kuzalisha umeme Zuzu.
Imetolewa na:
OFISI YA MKUU WA MKOA
DODOMA
Jan. 7, 2018
Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa
Anuani ya Posta: 914 DODOMA
Simu: +255 26 232 4343/232
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz
Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.