• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

AMANI YA NCHI YATAJWA KUWA AJENDA YA VIONGOZI WA SERIKALI NA WADINI

Imetumwa : July 13th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Suala la Amani katika nchi yetu ni ajenda ya kudumu kwa Viongozi wa nchi ya Tanzania kwani limekua likikumbushwa kila wakati ikiwa ni maelekezo ya viongozi wakuu wote wakiwemo wale wa Madhehebu ya Dini.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amebainisha hayo kwenye hotuba aliyoitoa kwa hadhara iliyohudhuria Kongamano la Amani Mkoa wa Dodoma lililoandaliwa na Idara ya Elimu Mahakama ya Kadhi chini ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Ofisi yake na kufanyika katika Ukumbi wa Sephil Sepphire Jijini Dodoma Julai 13, 2025.

“Suala la Amani ya nchi yetu limekua likikumbushwa mara kwa mara ikiwa ni maelekezo ya viongozi wetu wa Kitaifa kama ajenda ya kudumu ya viongozi wa nchi yetu lakini tumesikia pia viongozi wa Dini wakiongea juu ya Amani, kama tunayo dhamira ya kulinda Amani, kila mmoja kwa nia moja, basi Amani yetu itaendelea kuimarika”.

Aidha, Naibu Kadhi Mkuu na Mjumbe Baraza la Maulamaa Taifa Sheikh Ally Khamis Ngeruko amesema kuwa kuna haja ya kutazama Taifa lilipotoka na kutafakari yale waliyoyapitia wapigania Amani hasa kwa wanafunzi waliopo shuleni licha ya kusoma somo la Historia ya Tanzania ili waone umuhimu wa kuitunza Amani hii iliyopo.

Akiwasilisha Mada ya Umuhimu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi, Mkurugenzi wa Idara ya Uhuru wa Kidini na Mambo ya Kijamii Mchungaji Sabato Maseke amesema kuwa baada ya uchaguzi si muda wa kujali nani ameshinda au amepoteza bali ni muda wa kulingalia Taifa zaidi kuepusha Amani yetu kuingia katika migogoro.

Kadhalika, akimuwakilisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Galus Hyra, Kamishna Msaidizi wa Polisi Eva Stesheni, amezungumzia nafasi na mchango wa vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kuimarisha Amani nchini ambapo amesema vyombo hivyo vinahitaji ushirikiano kutoka kwa Wananchi kwani yote wanayotekeleza ni kwa mujibu wa Sheria.

Kongamano hilo limehitimishwa kwa kufikia maazimio kadhaa baada ya majadiliano ikiwa ni pamoja na; Sheria za mitandao zinatakiwa zieleweke kwa uzuri na ubaya wake, demokrasia iwe inapatikana wakati wote sio kipindi cha uchaguzi tu, kuheshimu na kutii Mamlaka halali kunaimarisha Amani na kujibidiisha katika shughuli kunaimarisha Amani.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA WAFANYABIASHARA WANAKUWA NA MAZINGIRA RAFIKI

    July 14, 2025
  • MZUMBE MBIONI KUANZA KAMPASI DODOMA

    July 14, 2025
  • AMANI YA NCHI YATAJWA KUWA AJENDA YA VIONGOZI WA SERIKALI NA WADINI

    July 13, 2025
  • DODOMA KUONDOKANA NA UKAME KUTOKANA NA UWEKEZAJI KATIKA MIRADI MIKUBWA YA UMWAGILIAJI

    July 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.