• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MALEZI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM/WALEMAVU NI JUKUMU LA JAMII NZIMA

Imetumwa : October 21st, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Inasemekana kuwa Jamii ina wajibu wa kulea makundi ya watu wenye mahitaji maalum au walemavu ili kuwawezesha kujikimu kimaisha kwa kupata mahitaji yao ya msingi kama ilivyo kwa watu wasio na mahitaji maalum/wasio na ulemavu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya nyumba ya makazi aliyoijengwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali kwa ajili ya Bw. Sospeter Chilumanga mwenye ulemavu wa viungo na familia yake katika eneo la Mvumi Makulu, Wilaya ya Chamwino leo Oktoba 21, 2025.

“Wajibu wa kulea Makundi haya yenye uhitaji au Walemavu ni wajibu wa jamii nzima ikiwa ni pamoja na Wazazi, Walezi, kijiji, Serikali kwa ngazi mbalimbali kutokana na uwezo unaokuwepo kwa wakati huo na pia ni wajibu wa mtu mmoja mmoja atakayeguswa, hakuna mtu mmoja mwenye jukumu la kulea watu wenye ulemavu”.

Kadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amesema jambo alilolifanya Mhe. Senyamule limegusa jamii nzima na kuweka alama kwa wasaidizi wake juu ya namna ya kuwahudumia wananchi na kuwagusa kulingana na nafasi zao pia limewafundisha wanajamii wanaoizunguka familia hiyo kuwa na Moyo wa kutoa.

Aidha, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Josephine Mwaipopo amesema Serikali ya awamu ya sita imetengeneza miundombinu na taratibu za kusaidia makundi maalum ikiwa ni pamoja na uwezeshwaji kiuchumi kupitia mikopo ya 10% ambapo wenye ulemavu wana 2% na mtu mmoja mmoja anaweza kupata mkopo huo.

Akitoa shukrani kwa msaada aliopatiwa, Bw. Chilumanga amemshukuru Mhe. Senyamule na wadau wote waliofanikisha kujengewa nyumba hiyo ambayo sasa itamhakikishia makazi bora na salama kwa familia yake huku akisema kuwa wapo wengi wenye uhitaji zaidi yake lakini ni Mungu tu aliyewagusa kumsaidia.

Nyumba ya Bw. Chilumanga imejengwa kwenye eneo lililotolewa na Serikali ya Kijiji cha Mvumi Makulu lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya 700 ambapo eneo hilo lipo jirani na huduma muhimu za kijamii kama shule, Kituo cha Afya, Soko na Ofisi ya Mtaa. Imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 28,513,000/= na ujenzi ulianza Agosti 24, 2025.


#DodomaFahariyaWatanzania

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigakura

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KILA ALIYE TUMIA MUDA WAKE KUJIANDIKISHA AKAPIGE KURA

    October 21, 2025
  • MALEZI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM/WALEMAVU NI JUKUMU LA JAMII NZIMA

    October 21, 2025
  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMETATUA KWA KIASI KIKUBWA KERO ZA WALIMU NCHINI

    October 18, 2025
  • DODOMA WAFANYA MAZOEZI YA AMANI KULIOMBEA TAIFA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

    October 18, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.