• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUJIUNGA NA MFUMO KURAHISISHA HUDUMA KWA WANANCHI

Imetumwa : June 17th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Rai imetolewa kwa Taasisi za Umma ambazo bado hazijaanza kutumia Mifumo ya huduma, kujiunga na  Mifumo hiyo kwani hayo ni maelekezo ya Serikali, kutokana na Mifumo hiyo kurahisisha utoaji huduma kwa Wananchi katika sehemu iliyofungamanishwa.

Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (MB), ametoa rai hiyo wakati wa hafla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye viwanja vya bustani ya Mapumziko Chinangali Jijini Dodoma leo Juni 17, 2025.

“Takribani Taasisi 185 ndio zimejiunga na Matumizi ya Mfumo, lakini zile ambazo bado, ziharakishe na kuhakikisha kwamba zinajiunga ili wananchi wapate huduma katika sehemu moja iliyofungamanishwa. Mifumo hii inatusaidia kurahisisha shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na e-WATUMISHI ambao unawapa watumishi haki zao kwa wakati”.

Aidha, Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Bw. Juma S. Mkomi, amesema umuhimu wa maonesho hayo ni wananchi wapate huduma za moja kwa moja kutoka kwenye Taasisi husika ikiwemo zile zinazoshughulika na masuala ya Afya sanjari na kufahamu majukumu ya kina ya Taasisi hizo.

Akitoa salamu za Mkao kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amesema Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ina jumla ya Watumishi 20,452 na kumekua na ongezeko la Watumishi ambalo linasaidia kuongeza kasi ya usimamizi wa Sera zinazotekelezwa na Serikali.

Siku ya Utumishi wa Umma Duniani ni Siku maalum ya Watumishi wa Umma ambayo husherehekewa kila ifikapo Juni 23 na Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi hao katika nchi zao ambapo maadhimisho hayo huambatana na maonesho mbalimbali ambayo huanza Juni 16.

Kaulimbiu:  “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchangia Uwajibikaji”.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAS MMUYA AWAAHIDI ZAWADI NONO WANAMICHEZO - UMITASHUMTA

    June 17, 2025
  • WAMILIKI WA MAABARA BINAFSI WATAKIWA KUTOA MAJIBU SAHIHI YA VIPIMO KWA WAGONJWA

    June 17, 2025
  • TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUJIUNGA NA MFUMO KURAHISISHA HUDUMA KWA WANANCHI

    June 17, 2025
  • DODOMA MOTO MKALI MASHINDANO UMITASHUMTA

    June 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.