• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIJANA RIKA BALEHE 13,218 MKOA WA DODOMA WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AHADI

Imetumwa : July 23rd, 2025

Na: Hellen M. Minja

       Habari - DODOMA RS

Mradi wa AHADI unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la 'World Vision Tanzania' kwa ushirikiano na Taasisi ya Tanzania Home Economics Association (TAHEA) unatajwa kuwanufaisha vijana rika balehe 13,218 wa Mkoa wa Dodoma kwa kuwafikia kwa elimu ya afya ya uzazi, kupinga ukatili wa kijinsia na stadi za maisha.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma CPA. Eric Ntikahera ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi wakati wa kikao cha uzinduzi wa mbinu ya uwezeshaji jamii katika utoaji wa elimu ya ukatili wa kijnsia kupitia viongozi wa madhehebu ya dini kilichofanyika katika ukumbi wa Mesuma Jijini Dodoma Julai 23, 2025.

“Mradi wa AHADI kwa kipindi cha miaka mitatu umekua na manufaa makubwa katika Mkoa wa Dodoma kwa kuwafikia kwa elimu ya afya ya uzazi, elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia na stadi za maisha jumla ya vijana rika balehe 13,218 ambapo 2,639 ni wale walio nje ya shule (Ke-1,394 na Me-1,245) huku 10,579 (Ke-5504 na Me- 5,066) wakiwa katika shule 20 za msingi na sekondari”.

Aidha, Mkurugenzi Mwandamizi wa World VisionTanzania Dr. Joseph Mayalla, amesema katika kipindi alichotumikia Shirika hilo, ameona mabadiliko chanya pale ambapo viongozi wa dini walipopewa nafasi ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi huu kwani wanatoa huduma mbalimbali kupitia nyumba zao za ibada ambazo huleta matokeo kwa haraka.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa TAHEA, Bw. Peter Mapunda kutoka Taasisi hiyo amesema Mradi huo umefanikiwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 409 kutoka Kata 10, vikundi vya vijana 138 vilifikiwa kwa elimu ya ujasiriamali, elimu ya utekelezaji wa bustani kwa vijana 363 wanaojiandaa kuingia kwenye malezi ya familia pamoja na vijana 2,639 waliunganishwa na kupatiwa huduma mbalimbali za afya.

Nae Bw. Kasei Msuya kutoka World Vision Tanzania, amesema mradi unalenga pia kuwafikia wazazi zaidi ya 274,000 na Viongozi wa madhehebu ya dini zaidi ya 2,110 waliopo Dar es Salaam na Dodoma hivyo, baada ya kikao hicho, viongozi hao watakua na jukumu la kufikisha taarifa kwa makundi hayo ili kuweza kuwafikia vijana wote waliolengwa.

Mradi wa AHADI unatekelezwa kwenye majiji ya Dar es salaam na Dodoma kuanzia Aprili 2024 hadi March 2029 ukilenga kuongeza utambuzi wa masuala ya afya ya uzazi na kuwawezesha kiuchumi Vijana Balehe wenye umri wa miaka 10-24 ambapo Mkoani hapa unatekelezwa katika Kata 12 za Chamwino, Nkuhungu, Mnadani, Msalato, Mkonze, Nzuguni, Kizota, Nala, Kikuyu Kusini, Kikuyu Kaskazini, Chang’ombe na Makole.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • VIJANA RIKA BALEHE 13,218 MKOA WA DODOMA WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AHADI

    July 23, 2025
  • MAAMBUKI YA UGONJWA WA HOMA YA INI ‘B’ YAFIKA 3.5% KITAIFA

    July 24, 2025
  • DODOMA NBC MARATHON YALENGA KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO

    July 24, 2025
  • NGO’s DODOMA ZATAKIWA KUWAJIBIKA KWA SHERIA NA TARATIBU

    July 23, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.