• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VITUO VYA AFYA KUSOGEZA HUDUMA ZA DHARURA JIRANI NA WANANCHI

Imetumwa : October 2nd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Ongezeko la Vituo vya kutolea huduma za Afya katika  Kata za Mkoa wa Dodoma linaonesha dhamira ya Serikali kurahisisha upatikanaji wa huduma za dharura karibu na wananchi pindi yanapotokea matukio ya ajali sambamba na kupunguza au kumaliza kabisa vifo vitokanavyo na uzazi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokuwa katika Kata ya Dalai kwenye ziara ya kikazi kutembelea miradi ya maendeleo ndani ya Wilaya ya Chemba Oktoba 02, 2025 ambapo alitembelea miradi ya miundombinu ya Elimu na  Afya.

“Uwepo wa Hospitali hapa utasaidia kuokoa maisha ya wananchi pindi inapotokea dharura ya ajali na matukio mengine kama hayo yanayohitaji huduma za haraka za kitabibu. Pia Serikali ina dhamira ya kusogeza vituo vya afya karibu na wananchi ili kupunguza au kumaliza kabisa vifo vya Mama na Mtoto, kila uhai wakati wa uzazi utunzwe”.

Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Dalai unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali kuu shilingi Milioni 678.7 pamoja na mchango wa nguvu za wananchi shilingi Milioni 10.8 na kufanya jumla ya shilingi Milioni 686.5, unalenga kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi hususan kina mama wajawazito na watoto.

Aidha, akiwa kwenye Mradi wa Zahanati katika Kata ya Songolo, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Halima Okash amesema mradi huo umegharimu shilingi Milioni 60 fedha kutoka Serikali kuu sambamba na Milioni 10 ambazo ni nguvu za wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali na umefikia 65% huku ukitarajiwa kukamilika Novemba 30, 2025.

Hata hivyo wananchi wa Kata ya Songolo hususan kina Mama ambao ndio wanufaika wakubwa wa mradi, wametoa shukrani zao kwa Serikali kwani kukamilika kwa Zahanati hiyo kutawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya kwenye Zahanati ya Kijiji  jirani cha Hamai.

Katika Mradi wa miundombinu ya Elimu, Mhe. Senyamule ametembelea ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa unaogharimu shilingi milioni 46 fedha kutoka Serikali kuu na ujenzi wa matundu 21 ya vyoo kwa shilingi milioni 49.4 fedha kutoka Mpango wa SRWSS kwenye shule ya msingi Mondo ambapo miradi hiyo inalenga kuboresha ufanisi katika ujifunzaji.

Akizungumza na wazazi katika Kata ya Mondo, Mhe. Senyamule ametoa rai kwao kushirikiana na Serikali kuhakikisha miundombinu ya kufundishia inaimarika sanjari na kupeleka watoto shule kwani hakuna Mtoto atakayeshindwa kusoma kutokana na mazingira kuwa mazuri na matarajio ya Mkoa ni kufanya vizuri kwenye matokeo ya Mitihani ya Taifa.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#nimejiandikishanitapigakura

#UmejiandikishaKapigekura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI INA DHAMIRA YA KILA MWANAMKE KUJIKOMBOA KIUCHUMI

    October 09, 2025
  • SACCOS NI FURSA KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA WANAWAKE

    October 11, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DODOMA

    October 09, 2025
  • KIWANDA CHA MVINYO KUFUFUA MATUMAINI YA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA

    October 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.