• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

AZZIM DEWJI KUINUA UCHUMI WA DODOMA KWA MITI YA MATUNDA

Imetumwa : February 3rd, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Katika muendelezo wa juhudi za kuikijanisha na kuipendezesha Dodoma kupitia Kampeni mbalimbali za upandaji miti, Mfanyabiashara maarufu nchini Bw. Azzim Dewji, amefika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuunga mkono juhudi hizo akilenga eneo la kuinua uchumi wa Wanadodoma kwa kupanda miti ya matunda.

Mfanyabiashara huyo amefika ofisini hapo leo Februari 03, 2025 akiwa na ujumbe ulioongozana nae ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alifanya kikao kifupi kwenye ukumbi wa Ofisi yake kwa kushirikisha wajumbe wachache ambao ni wadau wa ajenda ya upandaji miti katika Jiji hili.

“Mgeni wetu amenieleza dhamira yake kubwa ya kutaka kuungana na juhudi za Mhe. Rais hapa Dodoma za kuifanya Dodoma iwe ya kijani lakini ukijani wenyewe uambatane na uchumi wa wananchi wa Dodoma. Alisema anatamani kupanda miti ya matunda kwenye barabara ya kutoka Chamwino hadi Dodoma Mjini” Mhe. Senyamule

Mhe. Senyamule ameongeza kuwa hili ni jambo la Baraka kwa sababu limekutana na ajenda mbili za Mkoa ambazo ni ‘Dodoma ya kijani’ na ‘uchumi wa wananchi wa Dodoma’ kwani ukimpa mwananchi miche miwili ya miti ya matunda baadae akaanza kuuza, atakuza uchumi wake.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri, ameshauri zoezi la upandaji miti hiyo lifanyike kwa awamu mbili kwa matokeo chanya kwani upandaji miti ni zoezi moja lakini utunzaji wake unaweza kuwa changamoto hivyo awamu ya kwanza ipandwe miti mikubwa na awamu ya pili ipandwe ile iliyokua midogo kutoka kwenye vitalu.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Bw. Dewji amesema; Ardhi ya Dodoma inaweza kustawisha miti ya matunda kwa kiasi kikubwa na kuvuna huku, kupitia usafiri wa treni ya kisasa (SGR), uwezekano wa kuuzwa mikoa mingine ni mkubwa hivyo uchumi wa Mkoa na wananchi wake utakua kwa kasi kupitia biashara ya matunda.

Zoezi la upandaji miti ya matunda kwa hisani ya mfanyabiashara huyo, linatarajiwa kuanza mara moja kwenye kipindi hiki cha msimu wa mvua ambapo kwa Jiji la Dodoma, inatarajiwa kupandwa pembezoni mwa barabara kubwa, eneo la jeshi, pembezoni mwa mradi wa barabara za mzunguko wa nje, eneo la Mji wa Serikali, Mtumba, na kwenye barabara za Wilaya ya Chamwino.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.