• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

CHANJO DHIDI YA POLIO KUAZNA SEPTEMBA 21-24

Imetumwa : September 16th, 2023


Wizara ya afya imefanya mafunzo maalumu kwa wanahabari wa Mkoa wa Dodoma kuhusu kuanza kwa kampeni ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa polio inayotarajiwa kuanza kutolewa katika mikoa 6 nchini Tanzania ambayo ipo kwenye hatari zaidi ya kupata ugojwa huo kutokana na kugundulika kwa Mtoto mmoja katika Wilaya ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa.

Mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, yamelenga kuwaelimisha wanahabari taarifa sahihi za ugonjwa wa polio pamoja na namna utoaji chanjo unavyofanyika huku Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ambaye ametoa tathmini ya chanjo kimkoa na pia kuwaasa wananchi kupeleka watoto kupatiwa chanjo ya Polio

"Hali ya utoaji wa chanjo mbalimbali kwa watoto chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Dodoma ni nzuri sana, kwa takwimu za Aprili - Juni 2023 katika chanjo ya Penta ya 3, Mkoa umeweza kufikia lengo na kuzidi kwa asilimia 99 na katika chanjo ya Surua rubella, Mkoa umefikia lengo na kuzidi kwa asilimia 97. Hata hivyo, napenda kuendelea kuwakumbusha wananchi wenzangu katika Mkoa wa Dodoma kuendelea kupeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili waweze kupatiwa chanjo" Amesema Mhe. Senyamule.


Mkufunzi kwenye mafunzo hayo Dkt. Florian B. Tinuga ambaye ni Meneja Mpango wa chanjo, ameelezea kwa undani namna virusi vya Polio vinavyoweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na baadhi ya viashiria vya ugonjwa huo.

"Ugonjwa wa Polio unaambukizwa kwa njia ya mdomo kwa maana ya chakula au kinywaji kilichobeba virusi hivyo. Ugonjwa unapoingia mwilini unakwenda kudhoofisha Neva za fahamu hivyo inategemea ni Neva ya kiungo gani cha mwili kwani baadae kiungo hicho hupooza kabisa. Baadhi ya viashiria vya ugonjwa wa Polio ni kulemaa kwa ghafla, kukosa nguvu, kulegea viungo, kukosa nguvu na kushindwa kunyanyua mguu au mkono na Mtoto kushindwa kukaa. Nawasihi wananchi kuchukua tahadhari kujikinga na Polio" Amesema Dkt. Tinuga.

Takwimu zinaonyesha kuwa mgonjwa wa mwisho wa Polio kugundulika nchini ilikua Julai mwaka 1996 na kuanzia mwaka 1975 mpaka Sasa chanjo zilianza kutolewa kwa vipindi tofauti. Kwa sasa chanjo ya Polio inatarajiwa kutolewa katika mikoa 6 inayokaribiana na Rukwa ambayo ni Rukwa yenyewe, Mbeya, Katavi, Songwe, Kigoma na Kagera huku ikilenga Halmashauri 37 kutoka mikoa hiyo kwa idadi ya watoto 3,250,598 wenye umri kuanzia miaka 0 hadi 8. Chanjo ya Polio inatarajiwa kutolewa kuanzia Septemba 21 - 24 na watoa huduma watatembea nyumba kwa nyumba.


MWISHO


Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.