• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YASHEHEREKEA SIKU YA WAPENDANAO KWA KUPANDA MITI YA MATUNDA

Imetumwa : February 14th, 2025

Na:Sofia Remmi,

Habari-Dodoma Rs

Ikiwa ni muendelezo wa jitihada mahususi za kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa Kijani,leo Februari 14,2025 ,ambapo ni Siku ya Wapendanao, Ofisi  ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wa Mazingira, wamepanda miti ya matunda katika shule ya Sekondari Kisasa,kama namna mojawapo ya kusheherekea siku hiyo.

Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu Bw.Vicenti Kayombo ambaye pia amemuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dodoma,amesema kila mwanafunzi ana wajibu wa kusimamia miti hiyo ili kuhakikisha inakuwa vizuri.

Akizungumza na wadau waliojitokeza  Bw.Kayombo amesema miti 140 iliyopandwa leo itunzwe vizuri ili kutimiza lengo na adhma ya Viongozi wa Mkoa kukijanisha Dodoma.

“Wanafunzi waliopendekezwa kutunza miti hii niwasihi tunzeni miti hii kwani ina faida nyingi,mkizingatia kuwa ni miti ya matunda ,itawasaidia wanafunzi wote hapa mlipo.

Kupitia miti hii mtapata matunda,itunzeni huku mkizingatia pia kuwa Mkuu wa Mkoa  wetu ni kinara namba moja wa Utunzaji Mazingira.Miti hiii ikitunzwa vizuri wanafunzi wote mtafaidika na matunda yake” amesema Kayombo.

 Kwa upande wake Kiongozi wa wanafunzi katika Shule hiyo Joanitha Emmanuel amesema anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais  Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali  hata  kuwaletea miradi ya ujenzi wa madarasa ambayo  yamewezesha kuwepo kwa mazingira mazuri ya kusomea na kuahidi kuisimamia miti hiyo ili iweze kukua vizuri.

Tukio hilo la upandaji wa miti limewezeshwa  na taasisi ya Go-Plant-Tanzania ambayo ilitoa Miche ya miti ya matunda 140, kaulimbiu ikiwa ni “HUBA LANGU, MAZINGIRA YANGU”.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#kijanishadodoma

#hubalangumazingira yangu.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.