• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUJIFUNZA TEKNOLOJIA NA MIFUMO YA KISASA YA MAGARI

Imetumwa : September 2nd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Madereva wa Serikali wametakiwa kujenga tabia ya kujifunza mabadiliko ya teknolojia za kisasa za magari na mifumo ya namna ya usafirishaji kwa lengo la kuongeza tija na kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ulimwenguni hususan kwenye sekta hiyo ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokua akizungumza kwenye Kongamano la Nne la Madereva wa Serikali wa Tanzania lililoandaliwa na Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST) 2025 linalofanyika kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Septemba Pili, 2025.

“Mnalazimika kujenga tabia ya kujifunza mabadiliko ya teknolojia ya kisasa ya magari yetu na Mifumo mbalimbali ya namna ya kusafirisha magari yetu ikiwemo Mifumo ya kidijitali na ufuatiliaji. Endeleeni kujifunza mabadiliko haya ya Sayansi na teknolojia ya kisasa muende nayo sambamba”.

Kadhalika, akitoa salamu za Wizara, Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega amesema Madereva wa Serikali ni muhimili muhimu katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya Serikali kwani ndio wanahakikisha usafiri wa Viongozi na Watumishi unakua salama kiufanisi kuendana na hadhi ya Taifa letu.

Vile vile, Mdhamini wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ibrahim Juma amesema Wizara yake itatoa ushirikiano kwa kusimamia na kuhakikisha Mkutano huo utafanyika kwa ufanisi mkubwa Visiwani Zanzibar kama unavyofanyika Tanzania bara pale itakapohitajika kufanyika huko.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Serikali (CMST) Bw. Said Kabange amesema, wametekeleza maelekezo ya Mhe. Majaliwa ikiwemo kulinda nidhamu na wamelitekeleza kwa kula kiapo cha utii na kutunza siri za Serikali pia ameomba zoezi hilo la uapisho liwe endelevu kwa kufanyika kwenye mikoa yote nchini.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Madereva ni Askari wa kutunza Nyara za Serikali hasa Rasilimali watu kwani wanahakikisha wanasafirisha Watumishi wa Serikali na Wananchi wengine kwa umakini kutoka sehemu moja hadi nyingine hivyo kuendelea kuipa thamani Kada ya Udereva.

Chama cha Madereva wa Serikali kilianzishwa mwaka 2013 na kusajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2015 kwa namba SA20314 ambapo hadi sasa kina wanachama wapatao 8,387 ingawa Kongamano hilo la siku nne limehudhuriwa na wanachama 2500 kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara pamoja na Visiwani Zanzibar.

Kauli mbiu: “Dereva wa Serikali, Epuka ajali, Linda gari lako na Watumiaji wengine wa Barabara, Shiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025”.

 #dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WAHIMIZWA KUENDESHA KWA USTADI , KULINDA USALAMA BARABARANI

    September 04, 2025
  • ACC YATOA VIFAA VYA MILIONI 62 KWA WATOTO WENYE CHANGAMOTO YA AFYA

    September 04, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUJIFUNZA TEKNOLOJIA NA MIFUMO YA KISASA YA MAGARI

    September 02, 2025
  • TAASISI ZA KITAFITI TIBA ASILI ZASISITIZWA UFANISI WA VIWANGO VYA KIMATAIFA

    August 29, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.