• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

GUGU ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO CHEMBA

Imetumwa : May 2nd, 2023

Serikali Mkoani Dodoma imeendelea kuimarisha miundombinu katika sekta ya Elimu na Afya kwa lengo la kuboresha na kusogeza huduma kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 02/05/2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu alipofanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Chemba kukagua miradi ya maendeleo.

Bw. Gugu ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa, maabara na zahanati katika Vijiji vya Jangalo, Soya na Ombiri ambapo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho na umegharimu kiasi cha Shilingi millioni 90.6 kwa madarasa 12 na maabara 1, kwa upande wa ujenzi wa zahanati umegharimu kiasi cha Shilingi millioni 50.

"Ndugu zangu Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kukamilisha miradi hii ya maendeleo, nitoe rai kwenu kwanza kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati, pili miradi ikamilike kwa ubora wa hali ya juu” Gugu amesisitiza.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bi. Siwema Jumaa amesema mbali ya fedha kutoka Serikali kuu utekelezaji wa miradi hiyo ni pamoja na jitihada za nguvu za wananchi ambao kwa baadhi ya majengo ya zahanati na madarasa wananchi wamejenga maboma.

Pia, amewataka wakazi wa vijiji vya Jangalo ,Soya na Ombiri kuwa walinzi namba moja wa miradi hiyo kwa kuwa inaghariimu fedha nyingi za Serikali.

Ziara ya Bw. Gugu ilianzia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Chemba na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuongea na watumishi na kufanikiwa kukagua umaliziaji wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya Msingi Ombiri, ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa, jengo la Utawala, matundu 30 ya vyoo katika shule ya Msingi Soya, umaliziaji wa chumba 01 cha maabara shule ya Sekondari Jangaro na ujenzi wa Zahanati ya Mlongia.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu amefanikiwa kuongea na watumishi na kuwaasa kufanya kazi kwa weledi, ushirikiano, kupendana na kufanya kazi kwa ubora na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea .

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.