• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HOTUBA YA DKT. MAHENGE AKIFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA DODOMA

Imetumwa : January 21st, 2018

SALAMU ZA MKUU WA MKOA WA DODOMA DKT. BINILITH SATANO MAHENGE KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA DODOMA - CENTRAL PRESS CLUB (CPC) JANUARI 20,2018

Ndugu Abel Chidawali, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari,

Ndugu Wanahabari wa Mkoa wa Dodoma Makao Makuu ya Nchi yetu,

Ndugu Wageni Waalikwa.

Habari za Asubuhi.

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sisi sote Afya njema na kutuwezesha kukutana mahala hapa asubuhi hii ya leo. Pia, natoa shukrani zangu za dhati kwako binafsi Mwenyekiti na Viongozi wengine wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na Wanandishi wa Habari wote wa Mkoa wa Dodoma kwa ujumla, kwa kunipa heshima hii kubwa ya kuwafungulia Mkutano wenu wa Mwaka. Aidha, nakupongeza Mwenyekiti kwa kufanikiwa kuandaa Mkutano huu kwani naimani Mkutano huu ni kwa mujibu wa Katiba ya Chama chenu.

Ndugu Wanahabari,

Nakumbuka tulishawahi kukutana na kukaa pamoja kwa mara ya kwanza muda mfupi tu baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kunihamishia hapa Mkoani Dodoma Makao Makuu ya nchi yetu nikitokea Mkoa wa Ruvuma, nakumbuka tulitumia kikao hiko kufahamiana na kupanga mikakati ya Mashirikiano katika kufanya kazi kwa pamoja. Lakini hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki nanyi kwenye Mkutano wenu Mkuu, hivyo nimefarijika sana.

Naomba niseme kwamba tangu nimefika hapa Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Nchi yetu, Ndugu zangu Wanahabari mmenipa ushirikiano mkubwa sana kwenye majukumu yangu ya kila siku kama Mkuu wa Mkoa huu na nimeshuhudia Jeshi kubwa na Imara kabisa la Wanahabari, naomba nitumie fursa hii niwashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya hapa Mkoani Dodoma.

Ndugu Wanahabari,

Naomba kutumia fursa hii kuzungumza nanyi juu ya Dhamana kubwa tuliyonayo wana Dodoma katika Taifa letu, dhamana ambayo tumepewa na Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuihamishia Serikali na shughuli zake hapa Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Nchi yetu, tunafahamu Serikali yetu imeshahamia hapa Dodoma kwa maana ya kwamba Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mawaziri wote, Naibu Mawaziri Wote, Wakurugenzi wa Wizara na Watumishi wa Wizara wameshahamia hapa Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Nchi yetu na Mheshimiwa Rais naye ameahidi kuwa Mwaka huu atahamia hapa Mkoani Dodoma.

Dhamana hii ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi na Serikali kuhamia hapa Mkoani Dodoma kunawapa ninyi Wanahabari wa Dodoma kwa ujumla wenu jukumu kubwa la kuwahabarisha wananchi wote wa Tanzania na jumuiya mbalimbali za kimataifa shughuli zote za utekelezaji wa majukumu na mipango mbalimbali ya maendeleo ya Serikali na kuwawezesha kushirikiana kikamilifu na Serikali yao kwa kuwa wanapatiwa taarifa zote muhimu kwa usahihi.

Hivyo Ndugu wanahabari, Chini ya Mwenyekiti wenu, ninaomba mkae chini mjiwekee mikakati madhubuti ya kuona ni namna gani mnatoa mchango wenu wa habari kwenye jambo hili ambalo ni maendeleo makubwa kwa Taifa letu na ambalo hatukufanikiwa kulitekeleza kwa muda mrefu tangu miaka ya 1970.

Katika kuweka Mkakati wa ushiriki wenu katika kuwahabarisha Watanzania mtambue kuwa ninyi Wanahabari wa Mkoa wa Dodoma mnayo nafasi ya Kipekee kwa kuwa mpo hapahapa Dodoma kwa hivyo Watanzania wana matarajio makubwa ya kupata Taarifa zote za Makao Makuu kutokea kwenu ninyi Waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma na Sio Wanahabari wa Mikoa Mingine.

Hivyo lazima Mkakati mtakao uweka, Pamoja na Masuala mengine muhimu uzingatie masuala ya msingi yafuatayo:

ØMzingatie kuongeza sana WELEDI katika kazi zenu za kihabari mkitambua kuwa mnategemewa sana na jamii ya Tanzania hivyo msipozingatia jambo hili muhimu mtasababisha madhara makubwa kwenye jamii.

ØMzingatie sana NIDHAMU, UADILIFU NA UZALENDO kwenye kazi zenu za kila siku za kihabari, mtambuwe kuwa sasahivi hapa Mkoani Dodoma hamuhudumii Mkoa tu, Mnahudumia Serikali nzima na mnafanya kazi na Viongozi na Watendaji wa ngazi mbalimbali na kuwa sasa mmeongeza idadi kubwa ya wananchi wanaowafuatilia taarifa na kazi zenu, Aidha Mtambuwe kuwa ninyi ni Watanzania na Siku zote muitangulize Taifa lenu kwanza.

ØMkuze USHIRIKIANO Miongoni mwenu muwe kitu kimoja, mshirikiane kujadili changamoto zinazowakabili na fursa zilizopo na namna nzuri ya kuboresha utendaji kazi zenu. Pia mkuze mashirikiano na Wadau na Taasisi mbalimbali muhimu.

Katika hili Mimi kama Mkuu wa Mkoa, naahidi kuendelea kuboresha mahusiano kati yetu sisi Serikali na nyie Wadau wetu Wanahabari, Tutaendelea kuboresha Mazingira ili kuwarahisishia Ufanyaji kazi wenu na kushirikiana pamoja na nyie kutatua Changamoto zinazowakabili, Tayari tumeshaanza lakini tunaendelea mbele lengo letu tufike hatua ya juu ya ufanisi kwenye kazi zetu kwa pamoja sisi Serikali kwa Kushirikina na Nyie.

Tayari Wizara zote zipo hapa naimani Wizara yenu mama ya Habari na hususani IDARA YA HABARI MAELEZO inaendelea kuratibu vizuri kuhakikisha mahusiano mazuri na mashirikiano mazuri yaliyopo kati yenu Wanahabari na Serikali kwenye ngazi zote yanaendelea kuwepo na kuboreshwa zaidi na zaidi.

Nitoe Wito pia kwenye Mkutano muhimu wa Mwaka kama huu wa Wanahabari wa Dodoma Makao Makuu ya Nchi yetu, naonelea ni vema viongozi wa Makao Makuu ya Vyombo vyenu vya Habari wakaja kuhudhuria na kushiriki kikamilifu kwenye Mkutano kama huu kwa kuwa utawasaidia kutambua changamoto na Mazingira yenu halisi mnayofanyia kazi na hivyo watakuwa msaada mkubwa sana kwenu katika kutatua changamoto hizo na kuwaboreshea mazingira yenu kwa kuwa wanatambua kuwa wamewapa dhamana kubwa ya kuwakilisha vyombo vyao hapa Makao Makuu ya Nchi.

ØNitoe Wito kwa vyombo vya Habari vya Redio za hapa Dodoma Makao Makuu ya Nchi yetu (Nyemo FM, Rasi FM, AFM, Dodoma FM, Mwangaza FM, Kifimbo FM, Maisha FM, Uzima FM, Impact FM) oneni uwezekano wa kujitanua zaidi wigo wa kufikisha habari zenu kwa kuhakikisha mnaifikia mikoa mingi zaidi au nchi nzima kwa ujumla kwa matangazo yenu na kupitia teknolojia ya habari na mahusiano mfike hadi nje ya nchi kwa matangazo yenu. Mkisubiria kuamshwa mtashangaa vyombo vya nje ya Dodoma vimekuja na kuchukua nafasi yenu ninyi mkiwa mnaangalia hivihivi.

Ndugu Wanahabari,

Kabla Sijamaliza Salamu zangu, naomba niainishe masuala machache ambayo naomba Ndugu zangu Wanahabari Muendelee kutusaidia kutoa Taarifa, Elimu na kuhamasisha Wananchi wetu wa Dodoma Makao Makuu ya nchi yetu kwenye masuala ya msingi yafuatayo:

ØElimu kwa Wananchi wetu kujiepusha na UJENZI HOLELA na kuwa mabalozi wa kuzuia ujenzi holela, vibali vyote vya ujenzi na taratibu Rasmi zinatolewa na Mkurugenzi wa Manispaa na Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya zetu, Dodoma ni Makao Makuu lazima iendelezwe kwa kufuata Taratibu za Mipango Miji. Hii pia itazuia sana migogoro ya Ardhi.

ØKuhamasisha Wananchi Kushiriki katika jitihada za kunyanyua HALI YA ELIMU NA UFAULU kwenye Mkoa wa Dodoma.

ØKuelimisha na Kuhamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu katika KUONDO TATIZO LA NJAA NA UPUNGUFU WA CHAKULA kwa kuitikia na kutekeleza Mkakati wa Kilimo wa Mkoa kupitia kilimo cha mazao yanayotumia maji kidogo (Mtama, Uwele, Muhogo, Alizeti, Korosho, Zabibu n.k) na Matumizi ya Daftari la Kilimo.

ØKuelimisha na Kuhamasisha Wananchi wa Mkoa wa Dodoma kushiriki kikamilifu kwenye KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA NA USAFI WA MJI wetu wa Dodoma Makao Makuu ya nchi yetu ili kuwa na Makao Makuu bora zaidi Afrika na Maeneo Mengine Duniani, Hii itaendana Sambamba na Kampeni ya Upandaji miti aliyoizindua Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, pia itasaidia kuzuia Magonjwa ya Milipuko na Kuambukiza.

ØKutangaza fursa za Uwekezaji na Uchumi zilizopo kwenye Mkoa wetu wa Dodoma Makao Makuu ya Nchi na kuhamasisha wanadodoma kuzichangamkia bila kuzubaa.

Fursa kama Biashara za huduma na Biashara Mbalimbali ukizingatia Serikali imehamia, Uwekezaji wa Viwanda, Utalii kwenye maeneo Mbalimbali Kondoa Mpwapwa Kongwa nk,

Ndugu Mwenyekiti na Ndugu Wanahabari wote,

Nimalize salamu zangu kwa kurudia tena kukushukuru kwa dhati wewe binafsi Mwenyekiti, Viongozi wengine wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na Wanahabari wote wa Mkoa wa Dodoma kwa ujumla, kwa kunipa heshima hii kubwa ya kuwafungulia Mkutano wenu wa Mwaka, Nawatakia kila la kheri kwenye Mkutano wenu na Majadiliano Mtakayofanya, Na sasa Natangaza kuwa:

Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma Makao Makuu ya Nchi yetu (Central Press Club) - CPC Umefunguliwa Rasmi leo Januari 20, 2018.

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.