• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAADHIMISHO YA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI MKOA WA DODOMA DISEMBA 3, 2019

Imetumwa : December 3rd, 2019

DC Kondoa Mhe. Sezaria Makota awapongeza Watu wenye Ulemavu na kusisitiza jamii ihakikishe inawapa kipaumbele ili washiriki kuleta Maendeleo endelevu.

(Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma)

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota amewapongeza watu wenye ulemavu kwa namna walivyo mstari wa mbele kushiriki katika shughuli zinazochangia kuleta Maendeleo endelevu hapa nchini na hivyo kuondoa ile dhana potofu kwamba Watu wenye ulemavu ni tegemezi.

Katika kutoa fursa pana zaidi kwa Watu wenye ulemavu kushiriki katika shughuli za maendeleo, Mhe. Makota amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatenga asilimia mbili (2%) ya mapato ya ndani ya Halmashauri zao kwa ajili ya kuwakopesha watu wenye ulemavu ili waweze kuanzisha na kuendesha shughuli za kiuchumi na biashara ambazo zitawaingizia kipato na kuwapa uwezo wa kuchangia zaidi maendeleo ya nchi.

Ameyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani ambayo kimkoa (Dodoma) yamefanyika kwenye Wilaya ya Kondoa. Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katika Maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota amesema suala la Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga asilimia mbili (2%) ya mapato ya ndani ya Halmashauri zao kwa sasa ni suala la kisheria na siyo la hiari katika kuwatengea watu wenye ulemavu.

“Serikali ya Awamu ya tano ya Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli imeendelea kulisimamia hili kwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Fedha 2018 kwa kulifanya suala hili kuwa la Kisheria” alibainisha Mheshimiwa Makota.

Ametoa wito kwa watu wenye ulemavu kuendelea kuchangamkia fursa hiyo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye vikundi na kuwekeza shughuli za uzalishaji mali na uwekezaji mbalimbali kupitia mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri za Serikali za Mitaa ili kujiinua kiuchumi katika familia zao,Kaya na Taifa kwa ujumla. 

Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu - SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma limeipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutokuliacha nyuma kundi muhimu la watu wenye ulemavu katika mipango ya maendeleo.

Akitoa salamu za SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma Katibu wa shirikisho hilo Ndg. Justus Ng’wantalima amesema kuwa katika Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto wenye ulemavu wanaoandikishwa kujiunga na elimu ya awali, msingi na sekondari kupitia mpango wa elimu bila malipo na kusoma bure hadi kumaliza kidato cha nne huku wakipatiwa vifaa saidizi katika kusoma na kujisomea.

Ameongeza kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakijumuishwa kwenye kamati mbalimbali za maamuzi kama vile Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na Kamati za Wilaya (DCC); Kamati za UKIMWI za Halmashauri, Kamati za ulinzi wa mama na mtoto na nyingine nyingi. Amepongeza hatua za kuundwa kwa kamati za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya Mkoa hadi ngazi ya vijiji na mitaa na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kuteua watu wenye ulemavu kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi Serikalini.

Ameiomba Serikali kushughulikia tatizo la Ukosefu wa Takwimu halisi za watu wenye ulemavu ili mahitaji yao yaweze kujumuishwa na kushughulikiwa kwa ufasaha na ukamilifu kwenye mipango mbalimbali ya maendeleo. 


Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.