• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI MILIONI MOJA

Imetumwa : March 27th, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema suala la kupanda miti ni lazima na kuzitaka Halmashauri zote nchini kusimamia kwa karibu na kuhakikisha kwamba mazingira ya maeneo yao yanakuwa ya kijani, safi na ya kuvutia na zoezi hilo liwe endelevu.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa akizundua kampeni ya kupanda miti kitaifa kwa hisani ya Benki ya NMB ikishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), uzinduzi uliofanyika katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 27 Machi 2023. Amesema Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wanapaswa kutoa maelekezo kwa shule, taasisi mbalimbali na kwa wananchi ili washiriki kikamilifu katika uhifadhi na usafi wa mazingira.

Vilevile Makamu wa Rais ameziagiza Halmashauri kwa kushirikiana na TFS, kupanda aina za miti ambayo inaendana na mazingira ya maeneo waliopo pamoja na kuiwezesha jamii hususani ya vijana kupata elimu zaidi kuhusu utunzaji wa miti ili kuhakikisha wanachangia katika uhifadhi wa mazingira kwa weledi.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amemuhakikishia Dkt. Mpango kuwa wanaitunza miti kama ambavyo amekuwa akitoa maagizo ya kupanda na kutunza miti.

"Katika miti uliyopanda Dodoma hususan katika maeneo ya Ihumwa na Shule ya Msingi Msalato nikuhakikishie kuwa miti Ile inaendelea vizuri kwa 87% iko hai na Ile ambayo imekufa tumeirudishia ili ianze upya maana tunajua maelezo yako ni ya kupanda miti na unasisitiza zaidi kuitunza na sisi tunafanya hivyo lakini pia tumepanda miti 955,000 kwa mwaka huu na inaendelea vizuri amesema Senyamule

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema Benki hiyo itapanda miti milioni 1 kwa mwaka 2023 nchi nzima na kuitunza kuhakikisha inafikia lengo. Ameongeza kwamba Benki hiyo itaendesha shindano maalum la upandaji miti mashuleni litakalofahamika kama “kuza mti tukutuze” ambapo kupitia shindano hilo litakalofanyika kwa mwaka mmoja na nusu shule zitashindana kutunza miti watakayokabidhiwa na TFS.

Amesema pamoja na zawadi mbalimbali zitakazotolewa lakini pia shule itakayoweza kupanda miti 2000 na kukuza asilimia 80 na zaidi ya miti hiyo itafanikiwa kupata zawadi ya shilingi milioni 50. Bi Zaipuna amesema Benki ya NMB inatambua wajibu ilionayo katika jamii kuhakikisha wanatunza mazingira ili utendaji wa kazi kuwa mzuri na bora zaidi kwani mazingira yanapoharibika hakuna kundi linalobaki salama.

Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo amesema TFS itashirikiana vema na NMB kuhakikisha wanatekeleza vema adhma ya upandaji miti milioni 1 kwa kutoa miongozo mbalimbali ya kitaalamu na kushirikiana nao katika kila Nyanja kuhakikisha adhma hiyo inafanikiwa.

Aidha Prof. Silayo amesema ushirikiano baina ya NMB na TFS utasaidia katika kuongeza wigo wa upatikanaji wa miche ya miti jamii mbalimbali katika maeneo mbalimbali nchini na kuipanda kwa weledi kuhakikisha inastawi. Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidiana na serikali katika kuongeza nguvu kwenye uhifadhi katika kutekeleza kazi mbalimbali zinazopunguza utegemezi wa misitu na hasa kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa misitu, upandaji miti na kuhifadhi mazingira.

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo zaidi ya miti 3000 imepandwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.