• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MFUMO WA BARUA YA UTAMBULISHO WA MAKAZI KIDIGITALI (NaPA) WAZINDULIWA DODOMA

Imetumwa : February 8th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

Habari - DODOMA RS

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kutumia Mfumo wa Barua ya Utambulisho wa Makazi Kidijitali (NaPA), ulioanzishwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma na taarifa za makazi.

Mhe. Majaliwa amebainisha hayo kwa kutaja faida za matumizi ya Mfumo huo wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi iliyoanza Februari 06, 2025 na kuhitimishwa leo Februari 08, 2025 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.

"Mfumo huu unarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii, ulinzi na usalama eneo la Makazi, kuchochea uchumi na ukuaji wake, kuwezesha biashara kufanyika wakati wote na uwezo wa kukabiliana na majanga kwenye maeneo yetu. Hivyo basi, nchi yeyote, haiwezi kunufaika bila kuwa na Mfumo wa Anwani za Makazi". Mhe. Majaliwa.

Aidha, Waziri mwenye dhamana ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Silaa, amesema, maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi yanalenga kutoa hamasa kwa Taasisi na Wakazi kutumia Anwani kupata manufaa yaliyokusudiwa hivyo, Wizara inaendelea kusimamia Mifumo ya Utambuzi wa Watu, Biashara na Makazi.

Katika taarifa yake ya Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Mkoa huu Mhe. Rosemary Senyamule amesema,

"Mkoa wa Dodoma una minara ya mawasiliano 36 kati ya 758 iliyosimikwa Nchini na kwa upande wa Anwani za Makazi, awali, tulikua na Anwani 673,340, tukapata ongezeko la Anwani 59,147 na kufanya mpaka sasa Mkoa kuwa na jumla ya anwani za makazi 732,487 ambapo vyote hivi, vimewezesha urahisishaji wa mawasiliano ndani ya Mkoa"

Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu sambamba na uzinduzi rasmi wa Mfumo wa Barua ya Utambulisho wa Makazi Kidijitali (NaPA), yanatarajiwa kuwa endelevu kila mwaka kwani yatawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali ndani ya wiki hiyo ikiwemo kufahamu zaidi juu ya Anwani za Makazi.

Kauli mbiu: "Tambua na Tumia Anwani za Makazi kurahisisha Utoaji na Upokeaji wa Huduma"



#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.