• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MIRADI MIKUBWA YA KIMKAKATI KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU DODOMA

Imetumwa : April 20th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari - DODOMA RS

Mwenge wa Uhuru 2025 Mkoa wa Dodoma, unatarajiwa kupitia Miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa Mkoani hapa ambapo pia ni Makao Makuu ya Nchi. Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato, Ujenzi wa Barabara ya mzunguko wa nje, Mradi uliokamilika wa Treni ya mwendo Kasi SGR, Mji wa Serikali Mtumba na mingine mingi.

Hayo yamesemwa leo Aprili 20, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa hotuba yake ya kupokea Mwenge wa Uhuru 2025 katika uwanja wa CCM uliopo Kata ya Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa ambao utakimbizwa kwa umbali wa KM 1,333 kwenye Wilaya 7 na Halmashauri 8 za Mkoa kupitia miradi yenye thamani ya jumla ya shilingi 61, 105, 007,015.00.

Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameitaja miradi hiyo.

"Mkoa wa Dodoma una miradi mikubwa ambayo wanadodoma wanatakiwa kuifahamu, tuna Ujenzi wa Mji wa Serikali, Mtumba, ambao umefikia 70%, Ujenzi wa Treni ya mwendo Kasi SGR ambao ulifunguliwa Oktoba 2024, Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato, ambao umefikia 53% jengo la abiria, lakini 86% Barabara za kurukia ndege.

"Ujenzi wa Barabara ya mzunguko wa nje katika Jiji la Dodoma ambao upo hatua za mwisho za Ujenzi, Ujenzi wa skimu za umwagiliaji chini ya Programu ya 'Jenga kesho iliyo Bora', sisi tunayo miradi sita inayoendelea katika Wilaya mbalimbali za Mkoa, Ujenzi wa kituo cha michezo, Ujenzi wa uwanja wa Mpira wa miguu unaendelea kwa Bilioni 310, ukamilishaji wa Makao makuu ya mihimili ya Serikali, kituo cha kuondoa sumu kuvu kwenye mazao ambacho kimeongeza thamani ya mazao yanayouzwa nje ya Nchi.

Aidha, ameongeza, kuwa kupitia kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 yenye ujumbe Mkuu wa "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu", Mkoa umeshafanya kazi nyingi na unaendelea kuhakikisha kauli mbiu hiyo inatekelezwa ambapo baadhi ya mambo yaliyofanywa ni pamoja na;

Kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la mpiga kura, kuwahamasisha wananchi kutunza kadi ya mpiga kura, kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa wenye sifa, kushiriki kwenye Mikutano ya kampeni, kujitokeza kupiga kura na kujiepusha na vitendo vyenye kuashiria uvunjifu wa amani.

Mwenge wa Uhuru 2025 ambao umeanza rasmi mbio zake Mkoani Dodoma leo  Aprili 20, 2025 kwa kupitia  miradi 8 kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, unatarajiwa kutamatisha mbio hizo mnamo Aprili 27 na kukabidhiwa katika Mkoa wa Iringa Aprili 28, 2025. Wananchi wanaaswa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mbio hizo pindi zinapopita kwenye maeneo yao.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

#karibumwengewauhuru2025mkoawadodoma

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DHAMIRA YA MHE.RAIS , WATANZANIA KUPATA HUDUMA YATIMIA KWA MKOA WA DODOMA

    May 22, 2025
  • WAKANDARASI WASIOKAMILISHA MIRADI KUDAIWA FIDIA

    May 21, 2025
  • KUBORESHA LISHE NGAZI YA KAYA; KAMATI YA LISHE MKOA WA DODOMA YADHAMIRIA KUWA MFANO

    May 18, 2025
  • TANZANIA NCHI YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUZALISHA TANI 34,000 ZA ASALI

    May 20, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.