• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA DODOMA KUFANYA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU MACHI 21 HADI 22, 2020

Imetumwa : March 6th, 2020

Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, umepanga kufanya Kongamano la Wadau wa Elimu wa Mkoa kwa lengo la kuangazia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu kwenye Mkoa wa Dodoma na kusababisha kushuka kwa kiwango cha Elimu na hali ya ufaulu katika Mkoa.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Machi 6, 2020; Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema kuwa, kongamano hilo litafanyika tarehe 21 na 22 Machi, 2020 katika Ukumbi wa Mwl. Nyerere, Chuo cha Mipango, Dodoma. ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kuwa msukumo wa kuandaa Kongamano hili umetokana na ukweli kwamba hali ya maendeleo ya Elimu na ufaulu kimkoa sio ya kuridhisha. Ametaja viashiria vinavyoonesha na kupelekea kushuka kwa kiwango cha Elimu Mkoani kuwa ni pamoja na Watoto kutembea umbali mrefu kwenda shule na Watoto hawafundishwi vizuri kutokana na kukosekana usimamizi mzuri.

Aidha, amesema mwamko mdogo wa wazazi unasababisha wanashindwa kuchangia upatikanaji wa chakula cha wanafunzi wakiwa shuleni, changamoto ya miundombinu ya elimu kutotosheleza mahitaji na upungufu wa walimu.

“Mkoa unakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 6,768 kwa Shule za Msingi na vyumba vya madarasa 237 kwa Shule za Sekondari. Upungufu wa matundu ya vyoo ni 15,348 kwa Shule za Msingi na 1,829 kwa Shule za Sekondari” alibainisha Dkt. Mahenge.

Dkt. Mahenge aliongeza kuwa lengo la kongamano ni kuwakutanisha wadau ili kuchambua na kutambua hali halisi ya Elimu na changamoto zake katika Mkoa na hatimaye kuafikiana juu ya vipaumbele vya muda mfupi, wa kati na mrefu katika mkakati wa kuinua maendeleo ya Elimu na ufaulu wa Mkoa huku Kongamano hili likibeba kaulimbiu isemayo “Kuinua kiwango cha Elimu Mkoani Dodoma”.

Alitaja kuwa katika kongamano hilo, Mkoa utazindua kampeni endelevu ya ushiriki wa jamii katika uchangiaji wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu na samani za shule ili kuboresha zaidi mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji. Pia, itafanyika tathmini ya hali ya maono ya wananchi juu ya utayari wao wa kushiriki katika maendeleo ya Elimu. Kongamano litabainisha masuala ya kipaumbele ili kuweka mkakati wa muda mfupi wa kuinua Elimu katika Mkoa na kuamsha hamasa ya kujifunza na ufundishaji kwa kutoa tuzo kwa walioonesha juhudi za kipekee katika suala la maendeleo ya Elimu.

Amesema Kongamano litajumuisha uwasilishaji wa mada, mdahalo wa kina na maonesho ya Elimu huku likitarajiwa kutoa fursa kwa Mkoa wa Dodoma kushiriki kikamilifu katika kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, ambayo imeweka kipaumbele mahsusi katika kusukuma maendeleo ya Elimu nchini tangu iingie madarakani.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma Mwl. Maria Lyimo alisisitiza kuwa Kongamano linasisitiza Dhana ya Elimu msingi bila malipo na nafasi na wajibu wa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wa kushiriki kuwasimamia watoto kwenye elimu na kuchangia kujenga miundombinu ya elimu. Kongamano hilo litarushwa mubashara kupitia vyombo vya habari kama Luninga, Redio, Magazeti na Mitandao ya kijamii bila kusahau Shirika la Utangazaji la Taifa TBC.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.