• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AWATAKA WAKULIMA KUJISAJILI ILI WAWEZE KUFAIDIKA NA RUZUKU YA PEMBEJEO

Imetumwa : January 15th, 2025

Na. Sophia Remmi,

Habari - DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe Rosemary Senyamule amewataka wakulima ambao bado hawajajisajili,wajisajili ili waweze kufaidika na ruzuku inayotolewa na Serikali kwenye pembejeo za Kilimo.

Akizungumza wakati akitoa hotuba katika siku ya Mkulima Shambani  iliyofanyika leo Januari 15, 2025 katika makao makuu ya jeshi la Magereza yaliyopo Msalato jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa amesema;

"Niwasihi wakulima wote wa Mkoa wa Dodoma,kutumia mfumo wa Ruzuku ya Pembejeo. Ili kutumia mfumo huo, inakubidi kujiandikisha kwa wataalamu na kupata namba ambayo itatumika kununua mbegu na mbolea kwenye maduka ya wafanyabiashara waliojisajili katika mfumo. Wenzenu waliojisajili wanafaidika, wananunua mbolea kwa nusu ya bei".

Aidha Mhe Senyamule ameupongeza uongozi wa kiwanda cha mbolea cha ITRACOM kwa kutoa elimu  kwa Wakulima juu ya matumizi ya mbolea na faida zake.

"Niwapongeze tena ITRACOM kwa elimu hii nzuri na ni imani yangu kuwa wakulima mlioko hapa mtatumia mbolea hii na mkawe mabalozi wa kuwajulisha wenzenu, na tuone mabadiliko ya uchumi kwenu na kwa wananchi wengine".

Kadhalika Mhe. Senyamule, kwa niaba ya Serikali, ameuhakikishia Uongozi wa ITRACOM  kuwa wataendelea kuwapa ushirikiano kama ambavyo wamekuwa wakiwapa ili malengo ya pande zote mbili (Kiwanda na Serikali) yaweze kufanikwa.

Kwa upande mwingine, Mhe. Senyamule amewashukuru Jeshi la Magereza kwa kuanzisha shamba darasa ambalo limekuwa na matokeo mazuri. Sambamba na pongezi hizo, ametoa rai kwa wadau wengine wa Sekta ya Kilimo (Makampuni ya mbegu bora, makampuni ya mbolea za viwandani, jeshi la kujenga Taifa na makampuni ya viuatilifu, kushirikiana katika kutengeneza mashamba darasa mengine mengi ili wakulima waweze kupata elimu kwa kuona.

Katika hatua nyingine Mhe. Senyamule amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuvuta wawekezaji kuja kuwekeza Dodoma, amesema hilo limetokana na kuwepo kwa mazingira wezeshi ya uwekezaji.

Hafla hiyo ambayo Mhe. Senyamule alikuwa mgeni rasmi imelenga kuonesha ufanisi wa mbolea za FOMI katika uzalishaji na tija katika kilimo,mbolea ambazo zinazalishwa na kiwanda cha mbolea cha ITRACOM kilichopo katika kata ya Nala,halmashauri ya Jiji la Dodoma .

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.