• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

“Sifa ya Kiongozi ni Kuwaunganisha Watu Walio Chini Yake” RC.Senyamule , Chemba

Imetumwa : September 8th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Rosemary Staki Senyamule amefanya ziara Wilayani Chemba kwa ajiri ya kujitambulisha,kukagua miradi ya maendeleo na kisha kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Chambalo kilichopo Wilayani Chemba.

Akiwa Wilayani humo Mhe. Senyamule amepata fursa ya kukagua Mradi wa kituo cha afya na mradi wa maji, Kuzungumza na watumishi pamoja na wananchi  wa Chemba. Aidha Mkuu wa Mkoa alisikilioza kero za Watumishi na wananchi wa kijiji Cha Chambalo, ambazo nyingi ya kero hizo zilijikita katika masuala ya umeme, maji, miundo mbinu Barabara, Wodi ya wazazi,Upungufu wa Madarasa , Upungufu wa Walimu pamoja na Utawala Bora.

Mkuu wa Mkoa amewataka Wananchi na watumishi kutambua  kwamba miradi yote inayoendelea wilayani Chemba  ni miradi ya wananchi hivyo ni muhimu kila mwananchi kujua miradi na  maendeleo ya Kijiji Chao.Aidha, Mkuu wa Mkoa  amewataka Viongozi wa Halmashauri ya Chemba kuwajibika, na Kuwatembelea wananchi, kila kiongozi anapaswa kutambuliwa na wanakijiji, hakuna kitu kizuri kama wananchi kukutambua, kwani kwa kufanya hivyo wanakijiji wataanza kukupenda na kushirikiana pamoja katika ujenzi na maendeleo ya halmashauri na hata Kijiji.Ni vyema  wakandarasi  wa miradi mbalimbali ya maendeleo make ndelea kutoa taarifa na kuwaelimisha wananchi Kuhusu miradi inayoelendea katika maeneo yenu.

"Kushirikiana ni uamuzi kwa hiyo ninyi wenyewe kama viongozi  mnaweza kuamua kushirikiana. Na huku Serikalini hatuna fursa ya kuchagua wa kufanya nae kazi. Hivyo ni wajibu, kuangalia mazuri ya kila mtu na kuachana na mabaya yao. Kila mmoja aamue kushirikiana na wenzake.Sifa ya kiongozi ni kuwaunganisha watu walio chini yake ili wafikie lengo la kuwahudumia wananchi. Sote tuangalie namna bora ya kushughulikia na kuhangaika na tatizo. Siku tatu tembelea wananchi na siku 2 kaa ofisini hayo ni maelekezo ya Serikali.Halmashauri ziwatambue wenyeviti wa vitongoji na wenyeviti wa vijiji.Taarifa za fedha zitolewe kwa wakati kuwe na uwazi” Amesema  RC.Senyamule.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameahidi  kutoa mifuko 50 ya sementi itakayosaidia katika ujenzi wa wodi ya wazazi na kuwaagiza kumfahamisha pale uje nzi utakapoanza ili awaunge  mkono katika ujenzi. Pia Mkuu wa Mkoa amewasisitiza wazazi wa kijiji cha Chambalo kusomesha watoto wao.

Katika mradi wa maji Mhe.Senyamule amewaagiza wananchi wa Chambalo kupanda miti rafiki ya maji  kwani miti hiyo kuvuta maji. Mkuu wa Mkoa metoa namba ya simu ya bure ambayo wananchi wanaweza kuitumia kutoa malalamiko.  Aidha Mhe. Senyamule ameomba ushirikiano kwa kufanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa na kuwakumbusha wananchi kuwa kero  zote zifuate ngazi .                                  

Sambamba na hayo  Mkuu wa Mkoa amewpongeza Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba kwa kazi nzuri waliyoifanya wakati wa Mwenge kwani m,iradi yote ilipita, pamoja na ushirikiano mku bwa walioonyesha wakati wa sensa.

Kuhusu Changamoto ya Umeme. Mkuu wa Mkoa amewafahamisha Wanachemba kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani ameahidi kufikia mwaka 2025 kila Kijiji kitakuwa na umeme katika nchi ya Tanzania. Kila Kijiji kitakuwa na umeme. mradi wa  maji unaendelea zupo katika hatua za mwisho. Zamani kulikuwa hamna umeme wala maji iliigharimu wanakijiji kutembea umbali mrefu ili kupata hizo huduma lakinI serikali ya awamu ya sita imeweza kuwafikia takriban wanakijiJI ili kupata huduma hizo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Chacha aliwasii Watumishi na Viongozi wa Halmashauri ya  Wilaya ya Chemba,kufanya  kazi kwa  bidii na kwa ushirikiano.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.