• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TUANZE KUTUMIA NISHATI MBADALA KUPUNGUZA UKATAJI MITI - SENYAMULE

Imetumwa : December 31st, 2022

TUANZE KUTUMIA NISHATI MBADALA KUPUNGUZA UKATAJI MITI - MHE SENYAMULE

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa rai kwa wakazi wa Dodoma kuanza kutumia nishati mbadala ili kupunguza ukati wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa.

Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akiongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la chanzo cha maji cha Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kilichopo Ihumwa ikiwa ni mwanzo wa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti kwa Mkoa wa Dodoma.

"Leo tupo hapa kutekeleza mpango wa Serikali juu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni mwendelezo wa juhudi zilizoanzishwa na wenzetu. Nitoe rai kwa viongozi wa ngazi zote kuhakikisha tunasimamia maelekezo ya Serikali ya kuzuia ukataji miti bila vibali, tuanze kutumia nishati mbadala kama gesi kwa ajili ya kupikia kama anavyosisitiza rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan" Mhe. Senyamule alisisiza.

Vilevile, Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote katika Jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa wanasimamia na kuendeleza kampeni ya "Soma na Mti" kwa kuhakikisha kila shule na kila mwanafunzi anakua na Mti wake bila kujali kiwango cha elimu pia amesisitiza kufuatwa kwa Sheria ndogo ndogo zilizowekwa na Jiji kwa kila Kaya kupanda miti mitano kwenye eneo lake na kila anayenunua eneo ahakikishe amepanda idadi hiyo ya miti.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri aambaye ameshiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo amesema;

"Dodoma ina maeneo mengi ya wazi yanayohitaji kupandwa miti na sisi kama Jiji tunajitahidi kila kipindi cha msimu wa mvua tunapanda miti na kwa kipindi kilichopita tulifanikiwa kupanda takribani miti 800,000 kwenye maeneo mbalimbali. Upandaji miti kwenye eneo hili utaongeza thamani ya Mji wa Serikali na tuhakikishe madhumuni ya kupanda miti yanaendana na utunzaji wake" Alisisitiza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Shekimweri

Kadhalika, Meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Kati ambao ndio wadau wakubwa kwenye kampeni hii Bw. Mathew Kiondo, amesema mpaka sasa wana miche ya kutosha kwenye vitalu vyao takribani laki 8 hadi 9 inayosubiri kupandwa na mpaka Sasa wameshagawa miche 200,000 kwa wananchi na kuhakikisha kuwa hakutakua na upungufu kwani hata ikiisha hapo kwao, wataagiza kutoka sehemu nyingine.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa DUWASA amesema eneo la chanzo cha Maji cha DUWASA lililopo Ihumwa vijijini, lina ukubwa wa ekari 360 zilizotengwa kwa ajili ya hifadhi na linapatikana visima 15 vya kuzalisha maji ambavyo vinazalisha takribani lita 9,000,000 za maji na katika jitihada za kulihifadhi eneo hili pamoja na chanzo cha maji, Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na ujumbe wake wamepanda miti 2,000 katika eneo hilo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.