• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Ujumbe Toka Nchini Oman Watembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma

Imetumwa : July 26th, 2022

Hivi karibuni ujumbe wa Viongozi wanne kutoka nchini Oman, umetembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma kwa kusudi la kujitambulisha na kumsalima Mkuu wa Mkoa huyo. Ujumbe huo ulikuwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje Oman H.E Mohamed Bin Nasser Al Wahaibi,Balozi wa Oman Nchini Tanzania H.E Saud Al Shidhani, Injinia Luqman Mohamed Al Adawi pamoja na Mjumbe Bw. Zahir Sulaiman Najeem Al Abri.

Ujumbe huo umeongozwa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania, Nchini Oman Mhe. Balozi Abdallah.A.Kilima ambaye alifuatana na baadhi ya maafisa wa Ofisi ya mambo ya nje Tanzania, Bw. Leonce E. Bilauri_ Mkurugenzi Msaidizi idara ya Mashariki ya Kati- foreign pamoja na Bi. Florence Kebwe Desk officer Oman.

Akizungumza Balozi wa Tanzania Nchini Oman Mhe.Balozi Abdallah.A.Kilima ameeleza kuwa ziara ya viongozi hao toka Oman ni matokeo ya ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan nchini Oman. Ujumbe huu umekuja kutafuta sehemu ya kujenga Ofisi ya Ubalozi.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje Oman H.E Mohamed Bin Nasser Al Wahaibi ameeleza kuwa tumekuja Dodoma kwa sababu kubwa mbili, sbabau ya kwanza kutafuta kiwanja ambacho tutajenga ubalozi wa kisasa na sababu ya pili Tunataka kujenga kituo cha utamaduni/ cultural centre, lakini pia tumekuja kumtembelea balozi wetu mpya ambaye anaiwakilisha Oman nchini Tanzania.

Akizungumza Mhe. Mtaka ameukaribisha ujumbe wa Omani Makao Makuu ya nchi Dodoma na kuhakikishia kuwa Mkoa wa Dodoma upo tayari kuwapokewa nna kuwapatia viwanja. “Tunataka Mkoa wa Dodoma uonyeshe taswira ya makao makuu,na moja ya sehemu ambayo inafaa kwa uwekezaji.Tutawapatia na kuhakikisha mnawekeza Jijini Dodoma bila usumbufu wowote.Dodoma tuna fursa kwenye eneo la mifugo kama ng’ombe, mbuzi na kondoo.Aidha tunazalisha alizeti na Mtama. 50% ya alizeti inatoka Mkoani Dodoma.Hivyo ni vyema wawekezaji toka Oman wakaja na kuwekeza kwenye Nyanja ya kilimo au mifugo”.Amesema Mhe.Mtaka.

Nae Balozi wa Oman nchini Tanzania  Mhe, Saud Al Shidhani, amesema tayari mazungumzo yamefanyika na TIC/NARCO/TRA na tayari wamsaini MOU ya kufanya biashara pamoja. “Hivyo tutahakikisha wajumbe hawa wakija tena Tanzania wanafika Dodoma Makao Makuu”. Amesema  Mhe. Balozi Al  Shidhani.

Mwisho.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.