• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIJANA WAHIMIZWA KUJIKITA KWENYE KILIMO ILI KUKUZA VIPATO VYAO

Imetumwa : February 10th, 2025

Na,Happiness E. Chindiye

     Habari - Dodoma RS

Vijana Mkoani Dodoma wamehimizwa kujikita kwenye Kilimo  ili kukuza vipato vyao  na kuondokana na umasikini.

Akizungumza na washiriki Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya wakati akifungua Mafunzo kwa Vijana wabunifu wa Mkoani hapo kupitia mradi atamizi (Generation Food Accererator). Tarehe 10.02.2025 kwenye ukumbi wa Mesuma Hoteli Jijini Dodoma.

Bw. Mmuya amewasisitiza  Vijana hao kutumia fursa ya Kilimo kwani ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya nchi ikiongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkoa ya kukuza Uchumi wa mmoja mmoja.

“ Mnachofanya ni sehemu ya utekelezaji wa agenda ya Mkoa ya kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na njia moja wapo ni Kujikita kwenye kilimo biashara kwenye mazao ya Alizeti ,Mtama , mboga na matunda na mifumo jumuishi na endelevu ya chakula na lishe kwa Mkoani  hapa  .” Bw. Mmuya

Kadhalika ametoa wito kwa Vijana hao  na wanadodoma kwa ujumla kuendelea kupanda miti ya matunda na kufanya kilimo chenye Biashara kwani ataweza kuwatambua kwa matendo wakiendelea  kukua .

Naye Katibu  Tawala Msaidizi Sekta za Uchumi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Aziza Mumba amewasihi Vijana kujikita kwenye Kilimo na Ufugaji kwani ni ajira ya uhakika na fursa kwa nchi yetu kwani kuna rasilimali za kutosha.

Kwa Upande Wake Mshauri wa Program ya RIKOLTO Dodoma Bw. Willifaston Ntoroma amesema malengo ya mradi huo ni kuwasaidia Vijana kuzalisha chakula kingi na chenye ubora, kujipatia ajira na kujiwekea mifumo endelevu ya masoko.

Mradi huo unalenga vijana wa kiume na wanawake wenye umri wa miaka 18-35, unaotekelezwa kwa awamu ya kwanza (2024/2025) unajumuisha vijana 50 ambao watapewa elimu kwa siku sita huku wakiongozwa na kauli mbiu “ Kilimo biashara, pesa mfukoni “.


&&&


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#birthdayyangumtiwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.