• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAFUNZI 194 WALIOREJESHWA SHULENI WAENDELEA NA MASOMO DODOMA

Imetumwa : October 7th, 2024

Na; Happiness E. Chindiye

      Habari - Dodoma RS

Wanafunzi wasichana takribaini 194 Waliorejeshwa shuleni kutokana na changamoto za kupata ujauzito wameendelea na masomo kupitia mpango wa SEQUIP - AEP ( Secondary Education Quality Improvement Project) Mkoani Dodoma.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S. Mayeka wakati wa maadhimisho ya juma la Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Hogoro Wilayani Kongwa.

“Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali wasichana ambao  hawakuweza kupata Elimu ya Sekondari kwenye mfumo rasmi  kwa sababu mbalimbali ameamua kuwarejesha kupitia mpango wa SEQUIP-AEP (Secondary Education Quality Improvement Project).

“Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa  kuwarejesha shule wanafunzi wa kike 194 kupitia program hii na zoezi la kuendelea kuwabaini na kuwasajili linaendelea” Ameeleza Mhe. Mayeka

Ameongeza kwa kuwaasa mabinti wote ambao kwa bahati mbaya walikatiza au kukatiziwa masomo kwa sababu mbalimbali kuchangamkia fursa hiyo ya kujiendeleza iliyotolewa na Mheshimiwa Rais kwani elimu ndiyo silaha kuu ya ukombozi wa binadamu.

Naye Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Dodoma Mwl. Borase Itende Chibura amesema, kupitia utekelezaji wa programu ya MUKEJA, wananchi hawafundishwi tu Kusoma, Kuandika na Kuhesabu ( KKK) bali pia Stadi za maisha ili kuwawezesha kujikwamua Kimaisha.

"Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa miwili nchini inayotekeleza programu ya MUKEJA kupitia vituo viwili vilivyopo katika halmashauri mbili za Kongwa na Kondoa TC hali inayoongeza fursa ya upatikanaji wa elimu kwa watu wazima" Amesema Mwl. Chibura

Kwa Upande Wake Mshauri wa Maendeleo ya uwezo Bw. Matteo Mwita ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza ili kuweza kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu kwani ni haki ya kila mtanzania.

Maadhimisho hayo ya mwaka huu 2024 yameongozwa na kauli mbiu isemayo “Ujumuishi katika Elimu  bila Ukomo kwa Ujuzi, Ustahimilivu, Amani na Maendeleo.”

&&&

#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.