• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Yaliyojiri kwa Ufupi Wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Uandaaji Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2016/17 - 2020/21) wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma

Imetumwa : December 29th, 2017

YALIYOJIRI KWA UFUPI WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA UANDAAJI MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO (2016/17 - 2020/21) WA OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma inaendesha Mafunzo kwa Maafisa wake juu ya namna ya kuandaa Mpango Mkakati bora wa miaka mitano ambao ndio utakuwa dira inayoongoza utendaji wa Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma kwa miaka mitano kuanzia sasa (Strategic Plan 2016/17 - 2020/21)  

Mafunzo hayo ya Wiki mbili yanatolewa na Wataalamu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) ambao wana uzoefu mkubwa kwenye kuandaa mipango ya maendeleo ya maeneo mengi na kuandaa mipango mikakati ya taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi, Lengo la Mafunzo hayo ni kuwawezesha Wataalamu wa Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma kuandaa mpango Mkakati wa miaka mitano wa Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma baada ya mpango uliokuwepo awali kuisha muda wake hivyo kutoweza kutumika tena kwa kuwa umepitwa na wakati.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge ambapo katika ufunguzi amesisitiza masuala yafuatayo:


#Amewataka wataalamu wa Sekreterieti ya Mkoa wa Dodoma (RS Dodoma) kutambua kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi na tayari Serikali imeshahamia Dodoma kwa kiasi kikubwa na hivyo kuwa makini katika kupata mafunzo hayo ili waweze kutengeneza Mpango Mkakati wa miaka mitano kutokea mwaka huu ambao pamoja na masuala ya maendeleo lakini utazingatia kutoa huduma na ushirikiano mkubwa kwa Serikali ambayo imehamia.

#Amewataka wataalamu wa  RS Dodoma kuhakikisha wanajiwekea malengo yanayotekelezeka kwa kuwa wananchi wanahitaji kuona utendaji unaotoa matokeo chanya na yanayoonekana huku akiwataka kujikita katika vipaumbele na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2015 ya CCM, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/17 - 2020/21, Dira ya Maendeleo 2025, fursa mbalimbali na changamoto zilizopo Mkoani Dodoma.  

#Watumishi  wote wa RS Dodoma wanatakiwa kuuelewa mpango mkakati ambao utaundwa baada ya kukamilika mafunzo hayo kwa kuwa utatekelezwa na watumishi wote hivyo ili kwenda pamoja kila mtumishi atatakiwa kuuelewa vizuri.


#Katibu Tawala Mkoa ametaka mafunzo hayo kutumika vizuri kuwajengea uwezo  Wataalamu wa RS Dodoma ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji Sera na Mipango ya maendeleo ya Serikali.


#Imani yake kuwa hadi mwisho wa mafunzo, Dodoma itatoka na mpango mkakati wa mfano ambao hata mikoa mingine itakuja kujifunza.


# Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo hayo Dkt. Titus Mwageni kutoka Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini amebainisha kuwa Mkoa wa Dodoma una sifa ya kipekee ya kuwa Makao Makuu ya Nchi na kitendo cha Serikali kuhamia Mkoani Dodoma tayari ni fursa ya kipekee ambayo Mkoa wa Dodoma unatakiwa kuitumia katika kupiga hatua za kasi za maendeleo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.