• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

‘CAPITAL CITY DIPLOMATIC TOUR’ YAANZA KUZAA MATUNDA

Imetumwa : June 9th, 2025

*Balozi wa Oman Nchini akabidhiwa hati ya kiwanja kwa ajili ya kujenga kituo cha utamaduni Jijini Dodoma*

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Matokeo ya ziara ya Kidiplomasia ndani ya Jiji la Dodoma iliyofanyika Mei 27, 2025 yameanza kuonekana kufuatia Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Saudi Al Hilal Shidhani kukabidhiwa hati ya ujenzi wa kituo cha utamaduni cha Ubalozi huo kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la viwanja vya Mabalozi lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.

Hati hiyo iliyotolewa na Mkoa wa Dodoma,  ilikabidhiwa kwa Balozi huyo na Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Thabit Mahmoud Kombo katika hafla iliyofanyika June 05, 2025 kwenye Ofisi ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Mhe. Kombo amesema kituo hicho hakitakua tu mahali pa kuhifadhia na kuendelezea utamaduni, bali pia kitakua kivutio kwa Wanataaluma, Watafiti na Wanafunzi kutoka Mataifa mbalimbali hivyo, kusaidia kuongeza mapato ya Utalii na kuchangia kukuza uchumi wa Dodoma na Taifa kwa ujumla.

Naye Balozi huyo wa Oman Nchini  amemshukuru Mhe.Rais kwa kutoa kiwanja hicho,na kuongeza kuwa Serikali yake imeshajipanga kuanza mchakato wa ujenzi wa kituo hicho kitakachokuwa cha kisasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ambaye hivi karibuni aliandaa ziara ya Mabalozi (Capital City Diplomatic Tour) kutembelea miradi mbalimbali ya kimkakati iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na  Serikali Jijini hapa, ameeleza jinsi Mkoa ulivyojipanga kujenga mji janja ( Hombolo Thermatic City) kutenga eneo kwa ajili  ya tamaduni za makabila yote Nchini na nchi nyingine Duniani kwa kaulimbiu ya 'Take Dodoma to The World and Bring The World to Dodoma'na kuifanya Dodoma kuwa kati ya Majiji ya kisasa na ya kuvutia Duniani.Aidha amewakaribisha  wadau wengine kuja kuwekeza Dodoma .


#capitalcitydiplomatictour

#takedodomatotheworld

#bringtheworldtododoma

#dodomawerereadyforyou

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAS MMUYA AWAAHIDI ZAWADI NONO WANAMICHEZO - UMITASHUMTA

    June 17, 2025
  • WAMILIKI WA MAABARA BINAFSI WATAKIWA KUTOA MAJIBU SAHIHI YA VIPIMO KWA WAGONJWA

    June 17, 2025
  • TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUJIUNGA NA MFUMO KURAHISISHA HUDUMA KWA WANANCHI

    June 17, 2025
  • DODOMA MOTO MKALI MASHINDANO UMITASHUMTA

    June 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.