• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA KUONDOKANA NA UKAME KUTOKANA NA UWEKEZAJI KATIKA MIRADI MIKUBWA YA UMWAGILIAJI

Imetumwa : July 13th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia, imekuja na Mkakati wa kukuza Kilimo ambapo imewekeza katika Miradi mikubwa ya umwagiliaji kwenye Mkoa wa Dodoma na kuuondoa kwenye dhana ya ukame ambapo sasa kilimo cha umwagiliaji kinakwenda kuchukua nafasi na kuleta uhakika wa chakula wakati wote.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo sambamba na Ibada ya Kipaimara katika kanisa la Kianglikana Parishi ya Mwitikira katika Wilaya ya Bahi Julai 13, 2025.

“Mhe. Rais amekuja na mkakati mkubwa kabisa wa kukuza kilimo kwenye nchi yetu na sisi Mkoa wa Dodoma tumekua wa kwanza kupata miradi mikubwa ya kilimo ambayo imetufanya tuseme kumbe Dodoma sio kame kinachotakiwa ni maarifa. Maeneo mbalimbali yanachimbwa Mabwawa ikiwemo Bahi ambalo litamwagilia Heka 600”.

Aidha, Askofu wa Dayosisi ya Tanganyika ya Kati Rt. Rev. Dr. Dickson Chilongani (PhD), akiwa kwenye ibada ya wanafunzi wa Kipaimara, amewaasa wakazi wa eneo hilo kuachana na kilimo kinachohitaji mvua nyingi badala yake wajikite kwenye mazao yanayostahimili ukame huku wakijishughulisha na ujasiriamali wakati msimu wa kilimo unapokwisha.

Hata hivyo, Mhe. Senyamule amezindua miradi kadhaa iliyotekelezwa na Kanisa hilo kwa ufadhili wa Kanisa la St. Paul’s Richmond la nchini Marekani ikiwemo kisima cha maji ya kunywa chenye urefu wa Mita 50 kwenda chini kikiwa na uwezo wa kutoa maji lita 19,000 yatakayotumiwa na wakazi wa Kijiji hicho huku kikigharimu kiasi cha shilingi 75,484,558.

Mradi mwingine uliozinduliwa ni madarasa 9 na ofisi 1 ya Walimu katika shule ya msingi Mwitikira ambayo yamefanyiwa ukarabati wa kuwekwa sakafu, kupaka rangi, kupaua, kuweka madirisha ya chuma kwenye jengo la ofisi ya Walimu, kujenga varanda jengo la utawala ambapo ukarabati huo umegharimu kiasi cha shilingi 19,000,000.

Vile vile, Mradi wa shamba darasa la kilimo cha umwagiliaji ambao unalenga kuwafundisha wakazi hao kilimo cha mboga mboga pamoja na ujasiriamali umezinduliwa ukigharimu shilingi 16,356,000 wakati zoezi la utoaji matibabu bila gharama likiendelea kwa wakazi hao na wale wa vijiji vya jirani tangu Julai 10 ambapo mpaka leo wamehudumia jumla ya wagonjwa 660.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE APUNGUZA KERO ZA ARDHI KWA KIWANGO KIKUBWA MKOA WA DODOMA

    August 29, 2025
  • VIKUNDI 308 KUNEEMEKA NA BILIONI 3.6 ZA MIKOPO YA 10% DODOMA

    August 28, 2025
  • WATUMISHI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA KAZI

    August 26, 2025
  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.