• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

Imetumwa : May 8th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma umedhamiria kujikita kwenye ukuzaji wa uchumi kupitia kilimo cha matunda aina ya Tufaha (Apple). Hii ni kufuatia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule aliyoitoa alipotembelea Shamba Darasa lililopo eneo la Chinangali II Wilaya ya Chamwino linalozalisha matunda hayo Mkoani hapa kwa lengo la kujifunza uzalishaji wake.

Akiwa shambani hapo, Mhe. Senyamule alipata ufahamu wa namna tunda hilo linavyozalishwa na kutoa rai kwa wanadodoma kujikita kwenye uzalishaji wa tunda hilo adhimu Nchini ambalo hupatikana kwa wingi kwa kuagizwa nje ya nchi hususan nchini Afrika ya Kusini.

“Sisi kwa sababu zao hili halijalimwa katika Mikoa mingi kama zao la kimkakati, tukasema ili kupunguza ushindani na mikoa mingi, tuje na zao la Apple ambalo kwa sasa litakua linapatikana Dodoma. Majaribio ni haya tumeyaona ambayo hili hapa kwetu ni shamba darasa la Mkulima binafsi ambaye alianza kulima mwaka jana na ametusimulia jinsi alivyoona matokeo makubwa.”

Aidha, Mhe. Senyamule amezungumzia soko la Matufaha ambalo ni kubwa kutokana na wingi wake unaoingizwa kutoka nje ya nchi hivyo, endapo kama Mkoa wa Dodoma utafanya kilimo hicho, soko la kutosha linapatikana.

“Apple uzuri wake lina sifa nyingi, bado lina soko kubwa la ndani kwa sababu mengi tunaingiza kutoka nje ya nchi kwa sababu nchi yetu haijaweza kulima ya kujitosheleza, lakini lina soko kubwa la ndani, kama tukilima ndani ya nchi na ikashuka kidogo, bado itakua ni bei nzuri ya kumfurahisha Mkulima.” Ameongeza Mhe. Senyamule.

Aidha, Mkurugenzi wa ‘Mtimbi’s Farm’ Bw. David Mtimbi Mwaka ambaye shamba lake linatumika kama darasa kujifunza kuhusu kilimo cha Matufaha, ameelezea namna alivyoguswa kuanzisha kilimo hicho.

“Niliweka kama majaribio miche 100 nikawa navutiwa kuona kama itakua kama ‘apple’ ya South Afrika au itakua kama tulizozizoea za Tanga na sehemu nyingine? Baada ya kupanda niliambiwa zitaanza kuzaa baada ya miaka miwili na nusu, ili ikue vizuri unatakiwa kumwagilia na zilianza kuzaa katika kipindi cha mwaka mmoja hivyo inawezekana na zina ladha nzuri.”

Mbali na kutembelea shamba darasa hilo, Mhe. Senyamule alipata fursa ya kutembelea mradi wa kilimo cha umwagiliaji unaotekelezwa na kikundi cha Wanyausi Manchali ‘A’ kilichoanzishwa 19/12/2023 ikiwa ni mpango wa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo (BBT) kuwachimbia visima na kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima wadogo.

Mashamba hayo yamewezeshwa kwa kuchimbiwa kisima chenye urefu wa mita 160 kikiwa na uwezo wa kuhudumia mashamba 150 huku Bwawa likiwa na uwezo wa kubeba maji ujazo wa lita 850,000.  Mradi huo umesaidia kuboresha lishe kwa wakulima na jamii inayozunguka eneo hilo, kuongeza maarifa kwa kutumika kama ‘shamba darasa’ pamoja na kuimarisha kipato cha Wakulima.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.