• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"FUATILIENI MAENDELEO YA MIRADI YA SERIKALI" RC SENYAMULE

Imetumwa : October 6th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya ziara katika Halmashauri ya Kondoa DC lengo likiwa kukagua mradi wa ujenzi wa ofisi mpya ya Halmashauri, kuongea na watumishi pamoja na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Pahi, Kijiji cha Pahi kinachopatikana ndani ya Halmashauri hiyo.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameongozana na Wataalam wa Idara mbalimbali za Mkoa huku akilenga kutatua kero za Wazee, watumishi pamoja na wananchi wa Halmashauri hiyo. Akiongea na watumishi hao, Mhe. Senyamule amekazia suala la elimu kwa kusema kuwa suala hilo linahitaji kuwekewa kikakati zaidi.

“Dodoma tupo chini kielimu lakini Kondoa tupo chini zaidi, bado hatujadhamiria kuondoa ujinga. Naagiza kufanyike vikao vya wadau wa elimu kwa ngazi ya Kata na kila Kata ijitathmini na itengeneza maazimio yake. Nawapa mwezi mmoja hivyo vikao vifanyike na vije na mikakati ya kuongeza ufaulu, kuondoa utoro pamoja na kutatua changamoto ya miundombinu ya madarasa” Amesisitiza

Akipokea ripoti ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri kutoka kwa Mkuu wa divisheni ya Miundombinu, maendeleo ya mjini na vijijini Bw. Felchismi Tesha, Bw. Tesha amemueleza mkuu wa Mkoa kuwa mpaka sasa ujenzi wa Jengo hilo umekamilika kwa asilimia 70.Ujenzi wa jingo zima utagharimu Tshs. Bilioni 3.0 mpaka kukamilika kwake na Serikali kuu hutoa Tshs Bilioni Moja kwa mwaka hivyo mpaka sasa tumeshapokea Tshs Bilioni 2 na bado Tshs Bilioni 1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi.Ujenzi unatarajiwa kukamilika mwaka 2023.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Pahi, Kata ya Pahi kupitia mkutano wa hadhara na, Mhe. Senyamule amesikiliza kero zao mbalimbali zipatazo 21, ambapo nyingi ya kero hizo zilijikita katika masuala ya umeme, maji, barabara, elimu mikopo ya vikundi pamoja na fedha za TASAF.Mkuu wa Mkoa aliwaagiza wataalamu aliongozana nao kujibu kero za wananchi hao kulingana na sekta zao na hivyo kero zote kupatiwa majawabu.

Akizungumzia suala la fedha za miradi zilizotolewa na Serikali kuu kwa Kata hiyo, Mkuu wa Mkoa amebainisha kuwa Serikali kuu imetoa shilingi Milioni 934 kwa ajili ya mradi wa maji Kijijini hapo ambao bado haujakamilika, shilingi Milioni 500 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kwa ajili ya huduma za afya kwa mama na mtoto pamoja na Tshs. Milioni 46 za kumalizia ujenzi wa Zahanati.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa kwa upande wa elimu, Serikali kuu imetoa kiasi Tshs Milioni 46 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Kitoa iliyopo kwenye Kata hiyo,  na hivyo amewataka wananchi kufuatilia maendeleo ya ujenzi na kuhakikisha ukamilishwaji wa miradi hii kwani wao ndio wamepewa dhamana ya kusimamia na kuhakikisha inakamilika kwa ubora unaoridhisha kulinga na fedha iliyotolewa.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AFUNGUA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

    May 18, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.