• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO, MH. DKT FAUSTINE NDUGULILE (Mb) KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI YA UCHUNGUZI WA MABADILIKO YA AWALI YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NA MATITI MKOANI DODOMA

Imetumwa : January 22nd, 2018

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO, MH. DKT FAUSTINE NDUGULILE (Mb) KATIKA KAMPENI YA UCHUNGUZI WA MABADILIKO YA AWALI YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NA MATITI TAREHE 22 JANUARI, 2018, MKOANI DODOMA

Mkuu wa Mkoa Dodoma

Mganga Mkuu wa Mkoa Dodoma

Waheshimiwa Wabunge,

Viongozi mbali mbali mliopo hapa

Wafanyakazi wenzangu wa Sekta ya Afya,

Ndugu waandishi wa habari,

Wananchi wote,

Ndugu wa Wananchi

Habari za Asubuhi.

Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha sote kuwa hapa siku ya leo. Pia napenda kuwashukuru uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa kufanya maandalizi haya.Vilevile, ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kuwapongeza wote ambao mmejumuika nami katika uzinduzi huu, uwepo na ushiriki wenu unadhihirisha dhahiri dhamira yenu ya kuhakikisha kwamba jamii ya Kitanzania inahamasika na kuchangia katika juhudi za Serikali katika kupunguza tatizo la saratani kwa ujumla hususani saratani ya mlango wa kizazi na matiti.

Napenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa umahiri wake katika kuiongoza nchi yetu. Chini ya uongozi wake tumeshuhudia Serikali ikifanya mageuzi na maboresha makubwa katika sekta ya afya ambayo yameongeza ufanisi na tija kiwango kikubwa katika kuwapatia wananchi huduma za afya.

Aidha, ikumbukwe kwamba mwezi huu wa Januari ni mwezi wa kutoa elimu na kuhamasisha jamii kufanya uchunguzi wa mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi Duniani. Tunaungana na wengine kuhamasisha Jamii katika zoezi hili la kufanya uchunguzi na matibabu ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi. Wiki hii tutakuwa na upimaji huu kwa mkoa wa Dodoma na vilevile mkoani Njombe ambapo tunafanya kushirikiana na chama cha madaktari Wanawake (MEWATA).

Ndugu wa Wananchi

Takwimu za shirika la Afya Duniani (2012) zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya saratani ya mlango wa kizazi hutokea katika nchi zinazoendelea, ukilinganisha na nchi zingine za Afrika Mashariki, Tanzania inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wapya 50.9 kwa kila wanawake 100,000 na vifo 37.5 kwa kila wanawake 100,000.

Wanawake wengi hufika katika vituo vya kutolea huduma wakati ugonjwa umeshasambaa na hauwezi kutibika. Hii ni kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uelewa mdogo, elimu duni ya saratani, imani potofu juu ya saratani na matibabu ya saratani, hufanya watu wengi kushindwa kutambua na kugundua dalili au ugonjwa wenyewe mapema. Mwaka 2016 Taasisi pekee ya Saratani ya Ocean Road ilipokea wanawake 1934 wa saratani ya mlango wa kizazi. Takwimu hizi zimekuwa zikiongezeka sio tu kwamba kujua ukubwa wa tatizo, hii inatusaidia kuona jinsi gani jamii imeamka na kuhamasika kufahamu adhari za saratani na kuanza kuchukua hatua mapema.

Ndugu wa Wananchi

Wizara ilianzisha progamu ya kukinga na kudhibiti saratani ya njia ya uzazi mwaka 2008. Serikali Ilianzisha huduma za upimaji wa mabadiliko na matibabu ya awali mwaka 2002 kukiwa na vituo 3 katika vituo vyetu vya afya, hadi kufikia mwaka 2017 Disemba tuna vituo vya afya takribani 557 (443 vya serikali na 104 vya binafsi) ambavyo vinatoa huduma ya uchunguzi na matibabu ya mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi hapa nchini.

Vile vile,kuna hospitali 5 za Taifa/Kanda pamoja na hospitali 25 za Rufaa za Mikoa) zinatoa tiba ya upasuaji mdogo wa mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi “Loop Eletrosurgical Excision Procedure”. Mwezi Aprili 2018, Wizara itaanza kutoa chanjo dhidi ya kirusi kinachosababisha saratani ya mlango wa kizazi (Human Papilloma Virus) kwa wasichana kati ya umri wa miaka 9 mpaka 13.

Ndugu wa Wananchi

Rai yangu kubwa kwa wananchi ni kuwaomba kuanza kuhudhuria katika vituo vyetu vinavyotoa huduma hizi za uchunguzi wa mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi na matiti katika mikoa yote hapa Tanzania. Vile vile napenda kuwakumbusha Waganga wakuu wa Mikoa juu ya utekelezaji wa tamko langu la kuwataka kuhakikisha kila mkoa unatenga siku maalumu kila mwezi kufanya uhamasishaji na kufanya uchunguzi wa saratani za mlango wa kizazi na saratani ya matiti. Tumewapa malengo kila mkoa ili kuhakikisha kitaifa tunafikia wanawake Milioni 3 kufikia Disemba mwaka huu na huduma hizi.

Ndugu wa Wananchi,

Ni vyema basi kila mmoja wetu akapima afya yake mara kwa mara ili kutambua hali yake ya kiafya. Endapo utatambuliwa kuwa una dalili za ugonjwa wa Saratani tumia huduma za afya kulingana na ushauri utakaopewa na wataalam wa afya. Kwa wale ambao wameshajitambua kuwa na matatizo ya Saratani lakini hawatumii huduma za afya ipasavyo, nawaasa watumie huduma za afya zilizopo kwa manufaa ya afya zao na kuepusha athari zinazotokana na ugonjwa wa Saratani, kwani saratani ikigundulika mapema inatibika.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwahimiza wanawake wote kujitokeza kwa kwa wingi kupata huduma hizi, Saratani ya mlango wa Kizazi, na Saratani ya Matiti,uchunguzi huu unafanyika bure bila ya malipo yoyote.

Kwa kusema haya machache, niwatakie kila la kheri, na pia nawakumbusha tena wote kujitokeza kwa wingi kupima afya zetu.

Karibuni!

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.