• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE APUNGUZA KERO ZA ARDHI KWA KIWANGO KIKUBWA MKOA WA DODOMA

Imetumwa : August 29th, 2025

Kero za wananchi hasa zile za Ardhi, zinatajwa kupungua kwa kiwango kikubwa kutokana na jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Katibu Tawala Mkoa sambamba na Watumishi wa Ofisi yake ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Sululu Hassan.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa huyo alipokua akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma baina ya Katibu Tawala aliyemaliza muda wake Bw. Kaspar K. Mmuya na yule aliyeteuliwa hivi karibuni Dkt. Khatibu Kazungu katika ukumbi wa ofisi hiyo Jengo la Mkapa Jijini humu Agosti 29, 2025.


“Kwa Dodoma kazi yetu kubwa ni kutatua kero za wananchi, kero sizitatui mimi bali kwa kushirikiana na wasaidizi wangu wa kwanza akiwa RAS na Watumishi wote wengine wa Mkoa wa Dodoma. Zipo kero ambazo ni kubwa tunahangaika nazo, tumepunguza hasa kero za migogoro ya ardhi lakini hazijaisha”. Mhe. Senyamule.


Aidha, Katibu Tawala Mpya Mkoa wa Dodoma Dkt. Khatibu Kazungu amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa ushirikiano wa kutosha kwa kutimiza majukumu aliyopewa na Mhe. Rais huku akisisitiza uwajibikaji, juhudi na maarifa ili kuleta tija kwa Mkoa kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni (STK).


Hata hivyo, Katibu Tawala aliyemaliza muda wake Bw. Kaspar K. Mmuya amesisitiza suala la upendo na viongozi hasa Katibu Tawala Mpya kusimamia utekelezaji wa haki na maslahi ya Watumishi wao jambo ambalo katika utumishi wake alikua akilipa kipaumbele.


Hafla hiyo imekwenda sambamba na chakula cha pamoja kama ulivyo utamaduni kwa kila mwisho wa mwezi,ambapo  hujumuisha Viongozi na Watumishi wa Ofisi hiyo ikiambatana na kusherehekea kumbukizi za siku za kuzaliwa za  Watumishi waliozaliwa  mwezi Agosti kwa kukata keki na kufungua shampeni kama ishara ya upendo na umoja.



 #dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE APUNGUZA KERO ZA ARDHI KWA KIWANGO KIKUBWA MKOA WA DODOMA

    August 29, 2025
  • VIKUNDI 308 KUNEEMEKA NA BILIONI 3.6 ZA MIKOPO YA 10% DODOMA

    August 28, 2025
  • WATUMISHI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA KAZI

    August 26, 2025
  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.