• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

JENGO JIPYA LA HALMASHAURI YA MPWAPWA KUTATUA CHANGAMOTO YA HUDUMA KWA WANANCHI

Imetumwa : September 18th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa inatarajia kupata jengo jipya la Halmashauri na kutatua changamoto ya miaka mingi kwa Watumishi kutumia jengo lisilokidhi mahitaji yao hali iliyosababisha usumbufu kwa Wananchi pindi wanapohitaji huduma kutokana na kugawanyika kwa Ofisi zake.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Dkt. Sophia Kizigo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo iliyofanyika leo Septemba 18, 2025.

“Sisi Mpwapwa tunaishukuru Serikali kwa kutuletea fedha kiasi cha Shilingi Milioni 800 na baadae ilituongezea Bilioni 1 kwa ajili ya kuongeza Majengo zaidi ya kutolea huduma. Jengo la halmashauri linalotumika sasa ni la muda mrefu na halikidhi mahitaji na kusababisha baadhi ya Idara kupanga ofisi nje ya jengo, hali inayoleta changamoto katika utoaji wa huduma kwa Wananchi”.

Mradi mwingine uliotembelewa ni Ujenzi wa Ofisi ya Afisa Tarafa ya Mima ambao unagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 152 na umefikia 84% ya utekelezaji wake. Mhe. Dkt. Kizigo amesema kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha huduma kwa wananchi wa Tarafa hiyo ambao walikua wakitumia gharama kubwa kufika ofisini kwake Mpwapwa Mjini ambapo jengo lililokua likitumika awali lilijengwa mwaka 1956.

Aidha, Mradi wa ujenzi wa nyumba ya Watumishi na ununuzi wa vifaa tiba katika Kituo cha Afya Mima unaofadhiliwa na Shirika la KOFIH 2024/25 na kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 110, umefikia 98% za utekelezaji , ukikamilika utasaidia Watumishi wa Afya watano kupata Makazi.

Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imepokea jumla ya fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.6 kutoka Serikali kuu mwezi Juni 2025 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Ofisi za kutolea huduma ambazo zitasogeza huduma karibu na wananchi kwani ndio azma kuu ya Serikali.

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HOSPITAL YA BENJAMIN MKAPA YAADHIMISHA MIAKA 10 YA MAFANIKIO

    October 13, 2025
  • SERIKALI INA DHAMIRA YA KILA MWANAMKE KUJIKOMBOA KIUCHUMI

    October 09, 2025
  • SACCOS NI FURSA KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA WANAWAKE

    October 11, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DODOMA

    October 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.