• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAAMBUKI YA UGONJWA WA HOMA YA INI ‘B’ YAFIKA 3.5% KITAIFA

Imetumwa : July 24th, 2025

Na: Hellen M. Minja

       Habari - DODOMA RS

Maambukizi ya Ugonjwa wa Homa ya Ini aina ‘B’ yanatajwa kufikia  3.5% kulingana na utafiti wa Kitaifa uliofanywa mwaka 2022. Hayo yamebainishwa na Meneja Mapango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Magonjwa ya ngono na Homa ya Ini (NASHCoP) Dr. Prosper Faustine Njau wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jijini humu.

Mkutano huo umefanyika Julai 24, 2025 ukilenga kuutangazia Umma juu ya Maadhimisho ya siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo hufanyika  Julai 28 ya kila mwaka, na mwaka huu Kitaifa yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Morena Jijini Dodoma yakihudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri mwenye dhamana ya Afya Mhe. Jenista Mhagama (MB).

“Kulingana na utafiti wa Kitaifa uliofanywa mwaka 2022, ushamiri wa maambukizi ya Homa ya Ini ni ya aina ‘B’ ni 3.5% kwa watu wenye umri kuanzia miaka 15 mpaka 60. Tunaweza kuona ni tatizo kubwa kwa sababu kama ilivyo maambukizi ya Ukimwi Kitaifa ni 4.5% tunaweza kuona hapa Homa ya Ini inakaribia hapo”. Dr. Njau.

Aidha, ameongeza kuwa, Kitaifa wanalenga homa ya Ini aina mbili ambazo ni ‘B’ na ‘C’ambapo homa ya Ini aina C’ ushamiri wake ni 0.2% Kitaifa hali inayoonesha kuwa tatizo lake ni dogo ingawa ni hatari kupata ugonjwa unaoweza kupelekea kifo kwa haraka na hii imekua ikiwaathiri zaidi wale wanaotumia Dawa za kulevya.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dr. Nelson Bukuru amesema maadhimisho hayo kwa Mkoa yataanza Julai 26 hadi siku ya kilele Julai 28 ambapo shughuli mbalimbali za utoaji wa Huduma za upimaji afya zitafanyika katika viwanja vya zamani vya Mashujaa vilivyopo Jamatini Jijini humu.

Hata hivyo, ametaja huduma za afya zitakazotolewa katika kipindi hicho kuwa ni utoaji wa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Homa ya Ini, chanjo, upimaji na matibabu kwa wale watakaogundulika na tatizo hilo sambamba na kupatiwa rufaa itakapobidi ambapo huduma zote hizo zitatolewa bila gharama yoyote.

Sanjari na huduma hizo, pia zitatolewa huduma za uchangiaji damu salama, upimaji wa Virusi vya Ukimwi, magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu pamoja na elimu ya magonjwa mbalimbali hivyo wakazi wa Mkoa wa Dodoma wanakaribishwa kuhudhuria ndani ya siku tajwa ili kunufaika na huduma hizo.

Mpango wa kudhibiti Ukimwi, Magonjwa ya ngono na Homa ya Ini ni matokeo ya kuhuishwa kwa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi uliojulikana kama National AIDS Control Programme (NACP) ulioanzishwa 1988 kutokana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani la kujumuisha afua za homa ya ini pamoja na magonjwa ya ngono katika afua za VVU na Ukimwi.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • VIJANA RIKA BALEHE 13,218 MKOA WA DODOMA WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AHADI

    July 23, 2025
  • MAAMBUKI YA UGONJWA WA HOMA YA INI ‘B’ YAFIKA 3.5% KITAIFA

    July 24, 2025
  • DODOMA NBC MARATHON YALENGA KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO

    July 24, 2025
  • NGO’s DODOMA ZATAKIWA KUWAJIBIKA KWA SHERIA NA TARATIBU

    July 23, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.