• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAONESHO YA KILIMO NA MIFUGO NANE NANE KANDA YA KATI YAFUNGULIWA RASMI AGOSTI 3, 2017 KWENYE VIWANJA VYA MAONESHO NZUGHUNI NJE KIDOGO YA MJI WA DODOMA

Imetumwa : August 3rd, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati inayojumuisha Mikoa ya Dodoma na Singida Mheshimiwa Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wadau wote wanaohusika na Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati kuhakikisha Maonesho hayo hayatumiki kama sehemu ya kusafisha macho na kufanya utalii bali yawe Darasa na fursa ya kusaidia kuboresha shughuli za Wakulima na Wafugaji wetu na kuwafanya waongeze kipato kufikia kipato cha Kati.

Amewataka Wadau Waoneshaji kwa kushirikiana na Mamlaka zinazohusika kama za Mikoa na Halmashauri za Wilaya kuhakikisha wanawafikia Wakulima na Wafugaji kwenye Ngazi za Msingi na kuwasaidia waweze kuendesha shughuli zao katika njia bora na za kisasa za ufugaji na ukulima, lakini pia kuwapelekea teknolojia rahisi za kuchakata na kufungasha ili kuongeza thamani ya mazao yao na sio kuyauza yakiwa ghafi lengo kuu likiwa kumfanya Mkulima na Mfugaji kufikia kipato cha kati kinachochangiwa na uchumi wa viwanda kama Sera ya Maendeleo ya Nchi inavyosema.

Dkt. Nchimbi aliyasema hayo Agosti 3, 2017 wakati akifungua Maonesho ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Maonesho Nzuguni vilivyopo nje kidogo ya Mji wa Dodoma. Maonesho hayo yanashirikisha Mikoa ya Singida na Dodoma, lakini pia wadau mbalimbali kutoka mikoa mingine nao wamejitokeza kushiriki jambo linalofanya kuwa ya kuchangamka.

Amezitaka Halmashauri za Wilaya za Kanda ya Kati kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuwafikia Wakulima kwenye Ngazi za Msingi ili kuwawezesha mitaji ya kuendeshea shughuli zao za kilimo mifugo na uvuvi kwa masharti rafiki kabisa ili kuwawezesha kuendesha shughuli zao kisasa na kwa njia bora na teknolojia ya kisasa.

“Viongozi wa Wilaya za Kanda ya Kati na Halmashauri zake pamoja na wananchi (wakulima, wafugaji na wavuvi) mnaofika kwenye viwanja vya Maonesho ya Kilimo Nzuguni hakikisheni mnatembelea banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo kujionea, kwa kuwa wamewawekea aina nyingi za mikopo rafiki kwa ajili ya kupata mitaji ya kuendeshea shughuli zenu za kilimo, mifugo na uvuvi” alisema Dkt. Nchimbi.


Dkt. Nchimbi amebainisha kuwa Serikali inaendelea kupeleka umeme kwenye vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na umeme, lakini pia inajitahidi kuboresha miundombinu ya barabara na hivi karibuni Serikali imezindua wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) lengo ikiwa kuziboresha barabara za mijini na vijijini kuwa za viwango vya lami hivyo serikali inazidi kuweka mazingira bora ya uwekezaji na tayari wawekezaji wakubwa wameshaanza kujitokeza hususani wa usindikaji mafuta ya alizeti.

Jambo lililoonesha kumsikitisha Mkuu huyo wa Mkoa ni baadhi ya viwanda hivyo vya kusindika mafuta ya Alizeti kukosa mbegu za alizeti kwa ajili ya kukamua mafuta. Tatizo hili linaletelezwa na wakulima wetu kushindwa kuzalisha Alizeti inayotosheleza mahitaji ya Viwanda hivyo. Amesema haikubaliki wakulima wetu wanaendelea kuwa na pato duni wakati fursa ya kulima Alizeti na soko la uhakika kwenye viwanda hivyo lipo, hivyo, amewataka mamlaka zinazohusika na hususani Halmashauri za Wilaya Benki ya Dunia kuwawezesha wananchi kulima kwa tija na kuchangamkia fursa hiyo ya kulima Alizeti.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati Mheshimiwa Jordan Rugimbana amesema kwa mara ya kwanza maonesho ya Nane Nane yanasimamiwa na Serikali kupitia Sekretarieti za Mikoa baada ya TASO kufutwa na msajili wa Vyama vya Hiari. Kufuatia hali hiyo amesema kuanzia sasa kuna kila sababu ya kuyabadili sura Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati, yawe yenye tija zaidi na yenye kutoa fursa kubwa ya Elimu kwa wananchi/wakulima na wafugaji lkn pia yatoe kipato kitakachoboresha uratibu na usimamizi wake ili Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yawe Maonesho Bora na mfano kwa Kanda zingine.

Nae Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Nane Nane Kanda ya Kati Bi. Aziza Mumba alibainisha kuwa mwaka huu 2017 yanafanyika Maonesho ya kumi (10) katika uwanja wa Nzuguni. Kwa upande wa mifugo yanafanyika Maonesho ya saba (7) Kitaifa kuanzia mwaka 2011. Uwanja wa Nzuguni ni kituo cha kudumu kwa Maonesho ya mifugo Kitaifa. Amesema kwa miaka yote 8 ya nyuma, kulikuwa na mahudhurio makubwa ya watazamaji na waoneshaji.

Ametaja Kaulimbiu ya mwaka huu 2017 ni “ZALISHA KWA TIJA MAZAO NA BIDHAA ZA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI ILI KUFIKIA UCHUI WA KATI” akihusisha na Malengo ya Maonesho ya Mwaka huu kuwa ni utoaji wa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi. Wadau watajifunza kwa njia ya kuona, kujadiliana na kuulizana maswali. Maeneo makuu ya mafunzo ni teknolojia za uzalishaji wenye tija wa mazao, mifugo na usindikaji wa bidhaa kuongeza thamani. Teknolojia nyingine zitakazooneshwa ni hifadhi ya mazingira, vyanzo vya nishati mbadala, zana na pembejeo bora za kilimo na mifugo zipatikanazo nchini na teknolojia za mawasiliano.

Ameongeza kuwa Wadau pia wanajionea na kujifunza huduma zitolewazo na Serikali, Mashirika ya umma na binafsi, Aidha Maonesho hutumiwa na wafanyabiashara kuuza bidhaa, kufahamiana na kuingia makubaliano. Halikadhalika, watu wamekuwa wakipata fursa ya kuwaona baadhi ya wanyamapori katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.