• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MEI MOSI 2019 DODOMA: RC DKT MAHENGE KAMA RAIS MAGUFULI: - WAFANYAKAZI NI WADAU MUHIMU KUWEZESHA NCHI KUWA YA UCHUMI WA KATI IFIKAPO MWAKA 2025

Imetumwa : May 1st, 2019

MEI MOSI 2019 DODOMA: RC DKT MAHENGE KAMA RAIS MAGUFULI: - WAFANYAKAZI NI WADAU MUHIMU KUWEZESHA NCHI KUWA YA UCHUMI WA KATI IFIKAPO MWAKA 2025

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amewataka Wafanyakazi wote Mkoani Dodoma Makao Makuu ya nchi kutambua kuwa wao ni wadau muhimu na wanajukumu kubwa la kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Dkt. Mahenge amesema Wafanyakazi wanajukumu la kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, wanaongeza tija katika uzalishaji na utoaji huduma ili kuchangia kasi ya ukuaji uchumi huku wakizingatia uzalendo na uadilifu.

Ameyasema hayo leo hii wakati wa Maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Mei Mosi zilizofanyika Kimkoa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma zilizokuwa na kaulimbiu isemayo “Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora kwa wafanyakazi ni sasa”

“Hapa ninajumuisha wafanyakazi wote wa sekta za Umma, Binafsi na Wazalishaji wengine katka sekta kama Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Madini, Nishati, Biashara na Sekta za Huduma” Alibainisha Dkt. Mahenge.


Amesema Kaulimbiu ya Mei Mosi mwaka huu 2019 imekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia Sekta ya Viwanda na Sekta zinginezo za Uzalishaji zenye mchango katika ukuaji wa uchumi ifikapo mwaka 2025.

Katika kuelekea azma hiyo ya uchumi wa kati, Dkt. Mahenge amemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya Tano kwa jitihada za makusudi anazozifanya ili kufikia lengo hilo na akizitaja chache amesema kuwa hatua ya Rais Magufuli kuihamishia Serikali Mkoani Dodoma Makao Makuu ya nchi kijiografia ni katikati hivyo utoaji wa huduma kutokea Dodoma kutachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwenye kanda zote na mikoa yote hapa nchini kirahisi.

Amesema Mhe. Rais pia amekuwa na jitihada kubwa za ujenzi na uboreshaji miundombinu na Mazingira ya kuwezesha uchumi wa viwanda utakaotupeleka kwenye Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025 na kwamba jitihada hizo nikama Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Uzalishaji nishati ya Umeme utokanao na maji kwenye Maporomoko ya Mto Rufiji - Stieglers Gorge.

“Juzi tu tumeshuhudia Serikali imelipa takribani Shilingi Bilioni 688.65 kama malipo ya awali kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu unaojengwa kwa kipindi cha miezi 36 ambao utazalisha umeme kiasi cha MW 2115, kiasi hiki cha nishati ni kikubwa na kitawezesha kuhudumia viwanda vingi na kuchochea ukuaji uchumi” Alisema Dkt. Mahenge.


Aliongeza kuwa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Mwendo Kasi inayotumia Umeme (SGR), Ujenzi wa Reli hii kwa kipande cha Dar es Salaam Morogoro na Morogoro hadi Dodoma Stesheni ya Makutupora unaendelea na inatarajiwa mapema mwaka 2021 Reli hii kuwa imeshakamilika hadi Makutupora na kisha ujenzi wake kuendelea hadi utakapofika Mwanza na Kigoma na kusema kuwa Reli hii itakuwa na manufaa makubwa sana kwa shughuli za Viwanda na shughuli za uchumi kwenye ukanda mzima wa kati na nchi za Jirani kama Congo, Rwanda, Burundi na Uganda.

Dkt. Mahenge alibainisha kuwa, mbali na kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais kwenye ujenzi wa miundombinu ya Usafiri wa barabara, Uboreshji wa usafiri wa Majini na huduma za bandari, Mhe. Rais ameimarisha usafiri wa anga kwa kupitia Shirika la Ndege la Taifa ATCL kwa kununua ndege mpya nane (8) na uboreshaji wa viwanja vya ndege maeneo mbalimbali nchini akitolea mfano kuwa Mhe. Rais ametafuta fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya Ujenzi wa Uwanja Mkubwa na wa kisasa wa ndege wa Msalato jijini Dodoma.

Amehitimisha kwa kuwaeleza Wafanyakazi kuwa Miradi hii yote inayotekelezwa na Mhe. Rais Magufuli hapa nchini, ina manufaa Makubwa sana kwa nchi yetu na inachangia sana katika kuchochea ukuaji wa Viwanda na Uchumi. Amesema jambo hili litaiwezesha serikali kuongeza uwezo maradufu wa kuendelea kuboresha zaidi utoaji wa huduma za kijamii kama Elimu bora, huduma bora za Afya na pia kuboresha Mazingira na Maslahi ya Wafanyakazi hapa Nchini.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.