• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu Mpya wa MKoa wa Dodoma Kabidhiwa Ofisi

Imetumwa : August 4th, 2022

Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Sitaki Senyamule, leo amefanya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony Mtaka ambaye  kwa sasa ni Mkuu wa  Mkoa Wa Njombe.

Akiongoza makabidhiano hayo, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga amewapongeza wakuu hao wa mikoa ya Dodoma na Njombe kwa kuaminiwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ambae amewapatia Mamlaka ya kusimamia na kuendeleza kipande cha nchi. Aidha Dkt. Mganga amewaeleza watumishi wa mkoa wa Dodoma kuwa madhumuni ya kukutana ni kumpokea Mkuu wetu mpya wa Mkoa Mhe. Senyamule na hatimae kushuhudia makabidhiano ambayo atafanya na mkuu wa Mkoa anayeondoka Mhe. Anthony Mtaka.

Dkt. Mganga amemweleza Mhe.Senyamule juu ya mikakati na shughuli mbalimbali za Mkoa zilizo mbeleni ambazo ni pamoja na maonesho ya nanenane Kanda ya Kati yanayoendelea katika viwanja vya nanenane vya Nzuguni, Chanjo ya Uviko -19,na mbio za mwenge wa uhuru ambapo mwenge huo utapokelewa mkoani Dodoma 16/8/2022 na utakuwepo Mkoani Dodoma  hadi 23/8/2022.Sanjali na hayo Dk. Mganga amemfahamisha Mkuu huyo kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Dodoma ni takribani watu  2.7mln hii ni kulingana na sense ya mwaka 2012. Aidha Mkoa wa Dodoma una Wilaya 7, Halmashauri 8 na vijiji 822.

Akizungumza Mhe. Anthony Mtaka,ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, amemshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini na kumpa jukumu la kuongoza Mkoa wa Njombe. Mhe. Mtaka amempongeza Mhe. Senyamule kwa kuaminiwa na Rais kwa mara nyingine tena na kuja kuiongoza Dodoma. “Mwaka 2012 Mimi, Mhe. Senyamule na Mhe. Nawanda ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa tuliteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya, lakini leo wote tumekuwa Wakuu wa Mkoa,hili ni jambo la kumshukuru sana mwenyezi Mungu. Mhe. Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Dkt. Fatuma Mganga  ni mtu mwenye roho nzuri na mchapa kazi, pia una Wakuu wa Wilaya Wachapa kazi sana.Kwenye RS tulijenga timu, kwani Mimi nina amini sana kwenye vijana ambao wameemaliza chuo na kutafuta kazi.Hivyo nimekuwa nikitoa nafasi kwa vijana wengi sana waje kujifunza kazi na kupata mazoezi. Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa Wakati wote vipaumbele vyangu ni viwili tu ambavyo ni elimu na uchumi unaohusu watu. Hivyo kama tulivyofanya kazi kwa ushirikiano kwa kipindi cha mwaka mmoja basi  naomba mumpe ushirikiano huo huo Mhe. Rosemary Sitaki Senyamule”.Amesema Mhe. Mtaka

Aidha baada ya maelezo hayo Mhe.Mtaka amemkabidhi nyaraka mbalimbali Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma,nyaraka hizo zikiwa  ni pamoja na mpango Mkakati, Randama ya Mpango na bajeti pamoja na taarifa ya utekelezaji wa Chama Tawala.

Baada ya Makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary.S.Senyamule, amemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini. ‘’Nilijua kuhama nitahama ila sio Dodoma. Baada ya kuteuliwa kuja Dodoma nimekuja kutambua ya kuwa kumbe Dodoma sio Mkoa tu kama ilivyo Geita na mikoa mingine bali ni kwa makao Makuu ya Nchi. Na hivyo natakiwa kutimiza matazamio si ya wanadodoma tu bali ya Watanzania wote.Hivyo hii imani niliyopewa inakuwa na uzito wa aina yake. Pongezi kwa viongozi wote.” Amesema Mhe. Senyamule.

 Hongereni viongozi wote wa Mkoa wa Dodoma.Hongereni kwa kuwa na mpango mkakati wa miaka 5.Mhe Mtaka nimekuwa nikijifunza mengi  kutoka kwako nami nitaendelea kufanya hivyo.Hongera sana  kwa Machinga Module kwani ni mfano wa kuigwa kwa nchi nzima.Watumishi wa Dodoma niwasihi muendelee kufanya kazi vizuri hivyo hivyo kwani huu ni mkoa wa kiitifaki,kufanya kazi kwa bidii na maarifa kutasaidia sana kufikia  Dodoma inayotarajiwa na watanzania, Dodoma inayofanana na Makao Makuu ya Nchi. Tufanye Dodoma ambayo Mungu na Watanzania wanaitaka .Mwisho

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DHAMIRA YA MHE.RAIS , WATANZANIA KUPATA HUDUMA YATIMIA KWA MKOA WA DODOMA

    May 22, 2025
  • WAKANDARASI WASIOKAMILISHA MIRADI KUDAIWA FIDIA

    May 21, 2025
  • KUBORESHA LISHE NGAZI YA KAYA; KAMATI YA LISHE MKOA WA DODOMA YADHAMIRIA KUWA MFANO

    May 18, 2025
  • TANZANIA NCHI YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUZALISHA TANI 34,000 ZA ASALI

    May 20, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.