• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mwenge wa Uhuru 2017 wamaliza mbio zake Mkoani Dodoma Juni 27

Imetumwa : June 27th, 2017

Uongozi wa Serikali Mkoa wa Dodoma umeungana na Wananchi wa Wilaya Mbalimbali za Mkoa wa Dodoma kumuunga mkono na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya Tano kwa kuonesha Uzalendo Mkubwa na Jitihada zake za kusimamia Rasilimali za Nchi yetu na kudhibiti wizi na ubadhirifu wa Rasilimali za Taifa, hususani kwenye upande wa Madini.

Salamu hizi za pongezi zimetolewa kwenye maeneo mbalimbali na wananchi wa wilaya za Mkoa wa Dodoma wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 ambazo kwa Mkoa wa Dodoma zilichukua muda wa takribani wiki moja kuanzia Juni 19, 2017 na kuhitimishwa leo Juni 27, 2017 na kisha Mwenge kuendelea na mbio zake kwenye Mkoa wa Singida.

Akikabidhi Mwenge na Itifaki yake nzima kwa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana amemwomba Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Ndugu Amour Hamad Amour kumfikishia salamu hizo Mheshimiwa Rais Magufuli na kuongeza kuwa mbali na kumpongeza, Uongozi wa Mkoa na Wananchi wanamuombea Mheshimiwa Rais kwa Mwenyezi Mungu na wanamuunga mkono kwa kila Kiongozi kwenye Mkoa kuendelea kusimamia vema majukumu na wajibu wao kwa utiifu, uaminifu na uadilifu.

Mwaka huu 2017 kwenye Mkoa wa Dodoma Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwenye Wilaya zote saba (7) za Dodoma kwa umbali wa Km. 1375 na umepitia jumla ya miradi 55 yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 20 ambapo utekelezaji wake umefanikiwa kwa ushirikiano kati ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Wananchi na Wadau mbalimbali wa Maendeleo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.