• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

NANE NANE KANDA YA KATI KUZINDULIWA NA MHE. DKT. REHEMA NCHIMBI MKUU WA MKOA WA SINGIDA NA MWENYEKITI MWENZA WA KAMATI YA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA KATI AGOSTI 3, 2017

Imetumwa : August 2nd, 2017

Maonesho ya Kilimo na mifugo Nane Nane Kanda ya Kati yanayojumuisha Mikoa ya Dodoma na Singida yanatarajiwa kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Nane Nane Kanda ya Kati kesho Agosti 3, 2017. 

Maonesho hayo ya Nane Nane Kanda ya Kati yalianza Agosti Mosi lakini Uongozi wa Mikoa ya Dodoma na Singida uliamua kutumia siku ya Agosti 3, 2017 kufanya ufunguzi rasmi. Kadiri siku zinavyokwenda Maonesho hayo yanazidi kuchanganya kwenye Viwanja vya Nane Nane Nzuguni na idadi ya wananchi wanaokuja kwenye maonesho imeendelea kuongezeka siku hadi siku.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chemba ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Nane Nane Kanda ya Kati Mheshimiwa Simon Odunga imeeleza kuwa kwa sasa Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yanaratibiwa na kusimamiwa na Serikali za Mikoa ya Dodoma na Singida kufuatia Msajili wa Vyama vya Hiari kuifuta Taasisi ya TASO iliyokuwa ikisimamia Maonesho ya hayo. Tayari Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imeshatoa maelekezo rasmi kwa Serikali za Mikoa ya kusimamia Maonesho ya Nane Nane na imeahidi kuandaa mwongozo wa namna bora ya Serikali za kusimamia na kuendesha Maonesho hayo.

Kaimu Mwenyekiti Mheshimiwa Odunga amesema kuwa maonesho ya Mwaka huu yatajumuisha teknolojia mbalimbali za kilimo, Ufugaji na uvuvi. Aidha, yatakuwa na mashindano maalumu ya mifugo ambayo yatafanyika kwenye Arena Maalum ya Mifugo iliyopo viwanja vya Maonesho Nzuguni hapo Agosti 5, 2017.

Amesema Serikali inataka sera bora zilizopo kwenye sekta ya kilimo na mifugo sasa liwe ni jukumu la Sekretarieti za Mikoa katika kuzisimamia Halmashauri zake za Wilaya kuwezesha wananchi wao kufuga na kulima kisasa kwa kutumia pembejeo na zana bora za kisasa ili kuongeza tija ya uzalishaji kilimo na mifugo ili kuchochea ukuaji wa Sekta ya Viwanda kwa kuzalisha Malighafi ya kutosheleza viwandani.

Mheshimiwa Odunga ametoa wito kwa wananchi wa Mikoa ya Dodoma na Singida na maeneo mbalimbali ya nchi kuendelea kutembelea kwa wingi kwenye viwanja vya NaneNane Nzughuni Mkoani Dodoma ili kujionea na kujifunza masuala mbalimbali ya kilimo na mifugo, lakini amewataka kutembelea Banda la Maliasili na Utalii kujionea wanyama wa porini kama Simba, Chui, Nyati, Fisi, Mamba, Ndege mbalimbali na Nyoka wa aina mbalimbali. Amewataka watumie nafasi hii pia kujifunza utalii wa ndani ili kuchangia kukuza pato la Taifa. 


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.