• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA RELI YA KISASA KIPANDE CHA MOROGORO - DODOMA MAKUTUPORA

Imetumwa : March 14th, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 14, 2017 ameweka jiwe la msingi la kipande cha pili cha mradi wa Reli ya kisasa (Standard Gauge) kinachoanzia Mkoani Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika mradi huo zimefanyika katika Kijiji cha Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri, Manaibu Katibu Wakuu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mabalozi wa Uturuki na Uingereza hapa nchini, Wabunge na Wananchi wa Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa kipande cha pili cha Reli chenye urefu wa Kilomita 422 utagharimu shilingi Trilioni 4.3 na ni sehemu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya kati wa kuanzia Dar es salaam hadi mwanza yenye urefu wa Kilomita 1,219.

Bw. Kadogosa amesema ujenzi wa kipande cha pili utakaofanyika kwa miezi 36 utakamilika ifikapo Februari 25, 2021 na utatanguliwa na ujenzi wa kipande cha kwanza cha kuanzia Dar es salaam hadi morogoro utakaokamilika Novemba 2019.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa amesema wakati ujenzi wa kipande cha pili cha Reli ya kati ukianza, Ujenzi wa kipande cha kwanza umefikia asilimia 9 na kwamba treni zitakazotumia Reli hiyo zitakuwa na uwezo wa kubeba tani 10,000 za mizigo kwa wakati mmoja (sawa na malori 500 ambayo yangesafirisha mzigo kwa barabara) na itakuwa na uwezo wa kwenda kasi ya kilomita 120 kwa saa na Treni ya abiria kwenda kwa kasi ya Kilomita 160 kwa saa.

Kabla ya Kumkaribisha Mhe. Rais Magufuli, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amemshukuru kwa msukumo mkubwa aliouweka katika utekelezaji wa miradi na shughuli kubwa za Serikali ikiwemo ujenzi wa Reli na amewataka watanzania kuunga Mkono juhudi hizo.

Katika hotuba yake Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao amesema utasaidia kurahisisha na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo na abiria, na pia utaokoa barabara ambazo zinaharibika kutokana na kusafirisha mizigo mizito kwa magari.

“Kwa kutumia Reli hii mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi hapa Dodoma kwa saa 3 tu ikilinganishwa na saa 5 hadi 6 zinazotumika hivi sasa kusafiri kwa gari na pia mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa saa 9 ikilinganishwa na saa 36 anazotumia hivi sasa kusafiri kwa Treni” amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kusafirisha Tani milioni 17 za Mizigo kwa Mwaka ikilinganishwa na ya sasa yenye uwezo wa kusafirisha Tani milioni 5 tu.

“Bila shaka hii itaongeza mapato katika Bandari yetu ya Dar es Salaam na pia itaimarisha biashara hususani kati ya Nchi yetu na Nchi za Burundi, DRC, Rwanda na Uganda” ameongeza Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka wananchi wa Dodoma na Watanzania kwa Ujumla kuchangamkia zinazoletwa na mradi huu mkubwa ambapo utazalisha ajira za moja kwa moja 30,000 na zisizo za moja kwa moja 600,000 pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa barabara, bomba la mafuta la kuanzia Hoima - Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania, mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), Ukarabati wa Viwanja 11 vya ndege na ujenzi wa meli ya ziwa Victoria.

Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kulipa Kodi ili fedha zinazopatikana ziendelee kugharamia miradi ya Maendeleo ikiwemo kupeleka huduma muhimu za maji, elimu, afya na umeme ambapo Serikali imedhamiria ifikapo mwaka 2021 vijiji vyote nchini vipatiwe umeme.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AFUNGUA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

    May 18, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.