• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAS DODOMA AHIMIZA UENDESHAJI MFUMO ILIYOWEKWA NA COUNSENUTH KUPITIA MRADI WA LISHE KIJINSIA

Imetumwa : June 21st, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya ametoa maelekezo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, kuendeleza Mifumo iliyowekwa na Wadau wa Lishe ‘The Centre of Councelling, Nutrition and Health Care’ (COUNSENUTH) kupitia mradi wa Lishe kijinsia katika kuimarisha lishe, licha ya mradi huo kufika mwisho .

RAS Mmuya ameyasema hayo wakati wa kikao cha kufunga Mradi huo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jijini humu Juni 21, 2025.

“Hata hawa wakisema Mradi huu umefungwa, sisi tutaendeleza kwa sababu tunajua ‘Phylosophy’ ya Mradi, shughuli zilizopangwa na matokeo ya mradi tumeya ‘test’ na tumeyaona na sisi tunajivunia. Tunaposema leo udumavu umepungua kutoa 37.7% mpaka 24.4% maana yake mwakani nikisikia imepanda tena, kutakua na changamoto kwetu sisi wenyewe”. Alisisitiza RAS Mmuya.

Akitoa neno katika kikao hicho, Mshauri Mkuu wa Asasi ya COUNCENUTH Dr. Lunna Kyungu, amesema utekelezaji wa mradi huo katika Kata zote 26 na Vijiji 114 vya Wilaya ya Chemba, umekua na mafanikio makubwa kupitia ushirikiano na sekta za afya, elimu, kilimo, maji, mazingira na maendeleo ya jamii sambamba na ushiriki wa jamii yenyewe.

Kadhalika, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba Bw. Hassan Juma Mnyika ameishukuru COUNCENUTH kwa kazi kubwa waliyoifanya hususan katika kupunguza udumavu na kuahidi kuendeleza mazuri yote yaliyofanywa wakati wa Mradi huo kwani tayari wamewajengea uwezo wa kutosha.

Katika hatua nyingine,Afisa lishe Wilaya ya Chemba Bi. Faith Temu ametaja baadhi ya afua zinazotekelezwa na Mradi kuwa ni maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALIKI) inayotekelezwa kwenye vijiji vyote 114 pamoja na uongozi wa mguso katika vijiji 70 ambapo Viongozi wamejengewa uwezo kuweza kuguswa na changamoto za kijinsia zilizopo kwenye Vijiji vyao.

Asasi ya COUNSENUTH imetekeleza mradi wa Lishe Kijinsia katika Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha 2018 - 2025 chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Ireland ukiwa na lengo la kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ukiangazia umuhimu wa siku 1000 za mwanzo za Mtoto ambapo sasa umefungwa rasmi.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.