• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DKT. MAHENGE AMSIMAMISHA KAZI DAKTARI WA KITUO CHA AFYA BAHI KUFUATIA MALALAMIKO YA WANANCHI

Imetumwa : May 15th, 2018

MKuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameagiza kusimamishwa Kazi kwa Daktari Lucy Kashinde wa kituo cha Afya Bahi Sokoni ili kupisha Uchunguzi ufanyike dhidi yake kufuatia malalamiko waliyoyatoa Wananchi wa eneo hilo kwa Mkuu wa Mkoa huyo wakati wa Mkutano wake wa hadhara wa kuskiliza Kero za Wananchi kwenye eneo hilo.


Sehemu kubwa ya Malalamiko ya Wananchi kwenye Mkutano huo wa hadhara walimlalamikia Daktari huyo Kuwa amekuwa na Tabia za kuwafanyia ujeuri,lugha mbaya na utovu wa nidhamu Wananchi wanaofika kituoni hapo kupata huduma za Afya hususani wakinamama.

Wananchi wamedai Kuwa Daktari huyo hana kauli nzuri Kwa wagonjwa wanaofika kituoni hapo kupata huduma tofauti na madaktari wengine wa kituo hiko na tabia hiyo ni ya muda mrefu kwa Daktari huyo Jambo lililowafanya Wananchi kumuomba MKuu wa Mkoa Dkt Mahenge kuondoka na Daktari huyo baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.


Wakizungumza katika mkutano huo wa hadhara Bi. Mwasiti Masoud na Maria Damiani ambao ni Wakazi  wa Bahi Sokoni wametoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge wamemlalamikia Dkt. Lucy Kashinde kwa matumizi ya lugha chafu Na unyanyasaji kwa wagonjwa hususani kwa akina mama.

Uongozi wa Wilaya ya Bahi umethibitisha Kuwa na taarifa za malalamiko juu ya mtumishi huyo wa kituo cha Afya Bahi na kuwa MKuu wa Wilaya hiyo Mhe. Elizabeth Kitundu  alishamuita mtumishi  huyo  na kumuonya juu ya tabia hizo zilizolalamikiwa na Wananchi lakini bado tabia hizo ziliendelea na Wananchi wameendelea kumlalamikia Daktari huyo.


Kufuatia hali hiyo, MKuu wa Mkoa Dkt. Mahenge ameagiza kusimamishwa Kazi Kwa Daktari huyo na kuagiza Uchunguzi kufanyika juu ya malalamiko hayo na kumtaka MKuu wa Wilaya hiyo kusimamia Jambo Hilo na kumpelekea taarifa.


"Tuna uhaba wa Madaktari lakini hatuwezi kuwavumilia Madaktari watovu wa nidhamu" Dkt . Mahenge alisisitiza.

#ZIARARCDOMWILAYANIBAHI





Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.