• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DKT. MAHENGE HAJARIDHISHWA NA KIWANGO KIDOGO CHA WANANCHI KUANDIKISHWA KWENYE MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) ILIYOBORESHWA

Imetumwa : November 23rd, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema haridhishwi na kiwango kidogo cha wananchi walioandikishwa kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa kwenye Mkoa wa Dodoma na hivyo kuagiza kila Wilaya kuongeza nguvu zaidi katika kuhamasisha na kuandikisha wanachama wa CHF na hatimaye kila mwananchi aweze kutibiwa kwa mfumo wa Bima ya Afya.

Amesema Mfumo mpya wa CHF iliyoboreshwa ulianza kutumika kwenye Mkoa wa Dodoma tangu mwezi Julai 2018 ambapo kila kaya inalipia ada ya shilingi 30,000 kwa mwaka na hadi kufikia tarehe 20 Novemba 2018, jumla ya kaya 1467 tu ndizo zilizosajiliwa katika CHF iliyobororeshwa ambapo Halmashauri ya Bahi imesajili kaya 42, Chamwino kaya 101, Chemba kaya 55, Dodoma Jiji kaya 380, Kondoa Vijijini kaya 75, Kondoa Mji kaya 87, Kongwa kaya 298 na Mpwapwa kaya 429.

Mratibu wa CHF Mkoa wa Dodoma Dkt. Lutarara akitoa maelezo ya CHF iliyoboreshwa kwa Viongozi wa Mkoa wa Dodoma

Dkt. Mahenge alibainisha kuwa tangu Julai 2012 hadi kufikia mwezi Juni 2018 kabla mfumo mpya haujaanza kutumika, takwimu za Mkoa wa Dodoma zilikuwa zinaonesha kwamba idadi ya wanachama ambao walishawahi kujiunga na CHF ni kaya 156,721 sawa na asilimia 35% ya kaya 447,773, Kati ya kaya hizo, kaya 29,345 ndio kaya hai ambazo zinaweza kupata matibabu katika vituo vya kutolea huduma.

Kwa mujibu wa Dkt. Mahenge, viwango hivi bado ni vya chini sana na hivyo kuwaagiza viongozi wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na Halmashauri zake kuhakikisha kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 wahamasisha wananchi kujiunga katika CHF iliyoboreshwa ili kufikia lengo la Serikali la usajili wa asilimia 30% sawa na kaya 134,332 kati ya Kaya 447,773 zilizopo katika Mkoa wa Dodoma ifikapo Juni 2019. Pia, amewataka kuhamasisha wanachama ambao muda wa kutumia kadi zao za CHF umemalizika, walipie upya ada ya CHF ili waweze kupata matibabu kupitia kadi zao za CHF.

RC DOM Dkt. Mahenge akikagua vitabu vya Taarifa za CHF

Ametaka uhamasishaji wa wananchi ufanyike kijiji kwa kijiji na kuhakikisha Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji wanapata uelewa wa kutosha juu ya CHF pamoja na maboresho ya CHF yaliyofanyika kupitia Waraka Namba 1 kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili kusitokee upotoshaji juu ya mabadiliko ya gharama za uchangiaji wa mfuko wa CHF.

Maafisa wa CHF wakimuonesha RC Dom teknolojia rahisi inayotumia simu ya Mkononi kuwasajili wananchi kwenye CHF

Dkt. Mahenge ameyasema hayo yote mwishoni mwa wiki hii akiwa Wilayani Mpwapwa alipokuwa akizindua Rasmi kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa katika Mkoa wa Dodoma ambapo alisema kuwa Serikali ipo katika hatua ya kuhakikisha kwamba, inafikia malengo ya upatikanaji wa huduma bora za afya bila kuwa na kikwazo cha fedha kwa kuhakikisha wananchi wake wote wanapata matibabu bora kwa gharama nafuu kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa na hivyo kutoa wito kwa wadau wote wa Afya Mkoa wa Dodoma wakiwemo waheshimiwa Wabunge, viongozi wa dini na wadau wengine kutumia nafasi zao za ushawishi kwa wananchi kuhamasisha kila kaya kujiunga na CHF iliyoboreshwa.

RC Dom Dkt. Mahenge akikabidhi kadi za CHF iliyoboreshwa kwa Ndg. Hussein Rajabu wa Mpwapwa ambaye familia yake imejiunga na CHF iliyoboreshwa

“Ninawasihi wananchi wa Mkoa wa Dodoma kupokea kwa mtazamo chanya mabadiliko ya kiwango cha uchangiaji kutoka shilingi 10,000 kwa CHF ya zamani hadi shilingi 30,000 kwa CHF iliyoboreshwa kwa kaya ya watu 6 kwa mwaka” aliongeza Dkt. Mahenge.

Alisema matarajio ni kwamba ongezeko hili la uchangiaji litaboresha zaidi huduma zinazotolewa katika vituo vya Afya na kuwataka Waganga Wakuu wote wa Halmashauri kusimamia kwa ufanisi utoaji wa huduma katika vituo vya huduma za Afya.

RC Dom Dkt. Mahenge akikabidhi kadi za CHF iliyoboreshwa kwa Ndg. Photunate Elimanya wa Mpwapwa ambaye familia yake imejiunga na CHF iliyoboreshwa

Aliwataka Wakurugenzi Watendaji kuhakikisha taarifa za wanachama wote zinawekwa katika mtandao wa CHF-IMIS na makusanyo ya fedha yanawekwa katika akaunti ya CHF ya Mkoa kwa wakati na stakabadhi za kuwekea fedha benki ziwasilishwe kwa katibu Tawala wa Mkoa kila mwisho wa mwezi, pia aliwataka kufuatilia kwa ukaribu huduma za Afya zinazotolewa kwa wanachama na kama kuna changamoto zozote basi zitafutiwe ufumbuzi mapema ili zisiharibu taswira ya Mpango wa CHF. Aliwataka Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha vituo vya Afya vinatumia fedha hususani za dawa na vifaa tiba kwa mujibu wa taratibu na miongozo ili kusiwepo na taarifa kwamba kituo hakina dawa na wakati huo kina fedha katika akaunti yake.

Viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakiwapongeza wananchi waliojiunga na CHF iliyoborehwa

Dkt. Mahenge alimalizia kwa kuwataka Wakurugenzi Watendaji kuhakikisha kwamba kupitia bajeti za Halmashauri wanatenga fedha kwa ajili ya kuhuisha Kaya za wazee pamoja na kuendelea kuchangia wazee ambao hawana kadi za CHF hadi sasa.

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya zake waliohudhuria Ufunguzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye CHF iliyoboreshwa kwenye Mkoa wa Dodoma



Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya zake waliohudhuria Ufunguzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye CHF iliyoboreshwa kwenye Mkoa wa Dodoma


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.