• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DOM DR. MAHENGE AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI WA UGANDA MHE. MONICA AZUBA NTEGE

Imetumwa : June 6th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge leo Juni 6, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Nchi ya Uganda Mhe. Monica Azuba Ntege Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo Waziri huyo amepongeza jitihada za Serikali ya Tanzania za Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme - SGR.

Waziri Ntege amesema kuwa mradi huo wa Reli ya kisasa ya Umeme inayojengwa na Serikali ya Tanzania ina umuhimu mkubwa kwenye shughuli za kiuchumi na usafirishaji wa mizigo ikitokea bandari ya Dare es Salaam kuelekea ukanda wa ziwa Victoria kupeleka mizigo hiyo nchini Uganda; na kuwa inaweza pia kuhudumia nchi zingine za jirani kama Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Waziri Ntege pia amepongeza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Kaguta Museven wa Uganda na kusema kuwa ushirikiano huo utazinufaisha nchi hizi mbili kwenye nyanja mbalimbali za uchumi na maendeleo na kuongeza kuwa ipo haja ya Serikali yao ya Uganda kukaa na kuwafahamisha Wafanyabiashara wa Uganda namna watakavyonufaika na Reli ya Kisasa ya Umeme ya Mwendo Kasi-SGR inayojengwa hapa Tanzania mara itakapokamilika ujenzi wake.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amemfahamisha Waziri Ntege kuwa Jiografia ya Mkoa wa Dodoma kuwa katikati ya nchi inatoa urahisi wa kuzihuduma nchi za jirani kama Uganda, Rwanda, Burundi na jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ukilinganisha na mikoa kama Dar es Salaam.

Dkt. Mahenge ameongeza pia miradi ya ujenzi inayotekelezwa na Serikali kama huo wa Reli ya kisasa ya umeme na Mradi wa Uwanja wa ndege wa kisasa wa Msalato ambao tayari serikali inatarajia fedha za ujenzi wake zitatoka benki ya maendeleo ya Afrika na Mpango wa Mamlaka ya Bandari TPA kujenga Bandari Kavu Mkoani Dodoma; kwa apamoja miradi hii inazidi kuiongezea Mkoa wa Dodoma uwezo wa kuzihudumia nchi hizo za jirani kwa shughuli za kibiashara na uchumi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.